Loading...
title : LHRC YASIKITISHWA NA TUKIO LA KUCHOMEWA NYUMBA KWA MGOMBEA WA CCM HUKO TUNDUMA
link : LHRC YASIKITISHWA NA TUKIO LA KUCHOMEWA NYUMBA KWA MGOMBEA WA CCM HUKO TUNDUMA
LHRC YASIKITISHWA NA TUKIO LA KUCHOMEWA NYUMBA KWA MGOMBEA WA CCM HUKO TUNDUMA
Kituo cha Sharia na Haki za Binadamu kimesikitishwa na kitendo cha wananchi kujichukulia sharia mkononi kilichojitokeza katika kata ya Tunduma, Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya Tunduma na kuelezwa kuwa kitendo hicho uvunjaji wa sheria.Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Anna Henga akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Bi. Anna Henga alisema kuwa mgombea huyo alichomewa moto nyumba yake baada ya kuhama kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) na kuhamia Chama cha Mapinduzi CCM.
“Kituo cha Sharia na Haki za Binadamu kinakemea vikali kitendo hicho kwani kila mtu anahaki ya kuchagua, kuchaguliwa au kujiunga na chama chochote bila kujari hisia za watu wengine, hivyo kitendo cha kutishia maisha yake ni kukiuka haki za binadamu hususani haki kuu na ya msingi ya kuishi” alisema Anna Henga
Aliongezea kuwa kumekuwa na hali ya sintofahamu kwa wananchi katika kata zipatazo 30 ambapo wananchi wamepokonywa haki yao ya kuchagua viongozi katika uchaguzi mdogo wa marudio, Na ikielezwa kuwa baadhi ya wagombea hususani wa vyama vya upinzani wameenguliwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo tuhuma za kutokidhi vigezo vya kiufundi, na baadhi ya vigezo hivyo vimeelezwa kuwa kutojua kusoma na kuandika pamoja na vigezo vya kutokuwa raia wa Tanzania.
Wakati kwa mujibu wa ibara ya 13(4) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977 Imeeleza kuwa
“Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yeyote inayotekekeleza madaraka yake nchini ya sharia yeyote au katika utekelezaji wa kazi au shuguli yeyote ya mamlaka ya nchi” Mwisho wa kunukuu
Hivyo makala LHRC YASIKITISHWA NA TUKIO LA KUCHOMEWA NYUMBA KWA MGOMBEA WA CCM HUKO TUNDUMA
yaani makala yote LHRC YASIKITISHWA NA TUKIO LA KUCHOMEWA NYUMBA KWA MGOMBEA WA CCM HUKO TUNDUMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala LHRC YASIKITISHWA NA TUKIO LA KUCHOMEWA NYUMBA KWA MGOMBEA WA CCM HUKO TUNDUMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/lhrc-yasikitishwa-na-tukio-la-kuchomewa.html
0 Response to "LHRC YASIKITISHWA NA TUKIO LA KUCHOMEWA NYUMBA KWA MGOMBEA WA CCM HUKO TUNDUMA"
Post a Comment