Loading...

LUGOLA AIBANA KAMPUNI IRIS, AIPA SIKU 14 ITOE MAJIBU KULETA MTAMBO AU SHILINGI BILIONI 32 ZA NIDA

Loading...
LUGOLA AIBANA KAMPUNI IRIS, AIPA SIKU 14 ITOE MAJIBU KULETA MTAMBO AU SHILINGI BILIONI 32 ZA NIDA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa LUGOLA AIBANA KAMPUNI IRIS, AIPA SIKU 14 ITOE MAJIBU KULETA MTAMBO AU SHILINGI BILIONI 32 ZA NIDA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : LUGOLA AIBANA KAMPUNI IRIS, AIPA SIKU 14 ITOE MAJIBU KULETA MTAMBO AU SHILINGI BILIONI 32 ZA NIDA
link : LUGOLA AIBANA KAMPUNI IRIS, AIPA SIKU 14 ITOE MAJIBU KULETA MTAMBO AU SHILINGI BILIONI 32 ZA NIDA

soma pia


LUGOLA AIBANA KAMPUNI IRIS, AIPA SIKU 14 ITOE MAJIBU KULETA MTAMBO AU SHILINGI BILIONI 32 ZA NIDA

Na Felix Mwagara, MOHA 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameipa wiki mbili Kampuni ya Kimataifa ya Iris Corporation Berhard impe majibu ya kuwa italeta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au Dola za Marekani Milioni 14 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 32 za Tanzania. 

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma leo, mara baada ya kumaliza kikao na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na viongozi wa Kampuni hiyo, Waziri Lugola alisema kampuni hiyo haiwezi ikacheza na fedha za Watanzania ambao ni za walipa kodi. 

Lugola aliongeza kua lazima fedha hizo au mtambo huo upatikane kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haitakubaliana na mchezo mchafu wa aina yoyote, na pia yeye kama Waziri wa Wizara hiyo anaendelea kutekeleza maagizo ya Rais Dkt John Magufuli. 

“Tumezungumza nao na tumekubaliana nao kwamba tuwape wiki mbili ili bodi ya kampuni hiyo ikakae ifanye maamuzi ya aidha waturudishie fedha zetu au walete mtambo, lakini sisi kama nchi huu mtambo muhimu sana, bado tuna uhitaji, sisi tungependa baada ya hiyo wiki mbili wafanye maamuzi ya kutuletea mtambo,” alisema Lugola. 

Aidha, Waziri Lugola amewataka wamiliki wa kampuni zilizolipwa kifisadi fedha za Mradi wa mtambo wa NIDA kujisalimisha jijini Dodoma Agosti 3 mwaka huu wakiwa na mtambo huo vinginevyo warejeshe fedha zilizotumika. 

Pia Lugola ametoa agizo kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu na Mfanyabiashara Jack Gotham kufika ofisini kwake Agosti 3 saa 3:00 asubuhi ili kutoa maelezo yanayojitosheleza yatakayomsaidia kutoa maamuzi sahihi kuhusiana na ufisadi wa fedha zaidi ya bilioni 32 za mtambo huo ambao hadi sasa haujafika nchini. 

Lugola aliyataja kampuni hayo kuwa Gotham International ambayo imelipwa kifisadi shilingi 2,848,878,659.75, Iris Corporation Berhard ambayo imelipwa kifisadi 22,919,414,169,84, Gwiholoto Impex inayodaiwa shilingi 946,406,989,00, Sykes Travel Agent 5,979,600,00, Dk Shija Paul Rimoy 27,000,000,00, Aste Insurance 1,206,619.93, na Kampuni ya BMTL 569,192,090,00. 

Hata hivyo, Waziri Lugola aliwataka Watanzania kutowahusisha viongozi wa sasa wa NIDA na ufisadi huo kwa kuwa hawahusiki hata kidogo, matukio yote ya ufisadi yamefanywa na watangulizi wao na viongozi waliopo sasa wameletwa kuiongoza Mamlaka hiyo kwa ajili ya kuboresha utendaji wa NIDA. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao chake na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard. Viongozi wa kampuni hiyo wamepewa wiki mbili ili walete majibu kuwa wataleta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au shilingi bilioni 32 walizopewa na NIDA. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe alipokua akijadili jambo katika kikao alichokiitisha Waziri huyo kwa ajili kufanya mahojiano na Wamiliki wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard. Wapili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Shaiful Subhan, na Choong ambaye pia ni kiongozi mkuu wa Kampuni hiyo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard, Shaiful Subhan alipokua anafafanua jambo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, jijini Dodoma leo. Viongozi wa kampuni hiyo wamepewa wiki mbili walete majibu kuwa wataleta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au shilingi bilioni 32 walizopewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Watatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, Andrew Massawe. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao chake na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard. Viongozi wa kampuni hiyo wamepewa wiki mbili ili walete majibu kuwa wataleta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au shilingi bilioni 32 walizopewa na NIDA. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, Andrew Massawe, na wapili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Shaiful Subhan. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 


Hivyo makala LUGOLA AIBANA KAMPUNI IRIS, AIPA SIKU 14 ITOE MAJIBU KULETA MTAMBO AU SHILINGI BILIONI 32 ZA NIDA

yaani makala yote LUGOLA AIBANA KAMPUNI IRIS, AIPA SIKU 14 ITOE MAJIBU KULETA MTAMBO AU SHILINGI BILIONI 32 ZA NIDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala LUGOLA AIBANA KAMPUNI IRIS, AIPA SIKU 14 ITOE MAJIBU KULETA MTAMBO AU SHILINGI BILIONI 32 ZA NIDA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/lugola-aibana-kampuni-iris-aipa-siku-14.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "LUGOLA AIBANA KAMPUNI IRIS, AIPA SIKU 14 ITOE MAJIBU KULETA MTAMBO AU SHILINGI BILIONI 32 ZA NIDA"

Post a Comment

Loading...