Loading...
title : MAHAKAMA YAPOKEA BARUA YA KUFUTWA KAZI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU
link : MAHAKAMA YAPOKEA BARUA YA KUFUTWA KAZI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU
MAHAKAMA YAPOKEA BARUA YA KUFUTWA KAZI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea barua ya kufutwa kazi kwa aliyekuwa Mhasibu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), Godfrey Gugai kama kielelelezo namba sita katika kesi ya utakatishaji na kumiliki mali isiyolingana na kipato chake inayomka bili Gugai na wenzake watatu
Uamuzi huo umetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kutokana na pingamizi la upande wa utetezi waliokuwa wanapinga shahidi wa kwanza wa upande wa Jamuhuri kutoa kielelezo hicho wakidai kuwa siyo mtu husika.
Katika pingamizi lao Wakili wa utetezi Alex Mgongolwa alidai mahakamani hapo kuwa, shahidi Huyo hapaswi kutoa kielelezo hicho kwa kuwa siyo mtu aliyeandika barua hiyo na wala haielewi vile vile hakikuwa mikononi mwake.
Akitoa uamuzi wa kupokea kielelezo hicho, Hakimu Simba amesema, kifungu cha 34(b)(1) walichotumia upande wa utetezi kuwasilisha pingamizi hilo hakiusiani kabisa na mazingira ya kesi hiyo,"Shahidi Huyo Ayoub Akida katika ushahidi wake alidai yeye ni afisa Utumishi Mkuu wa Takukuru, ambaye ndie anahusika katika kutunza mafaili ya wafanyakazi ikiwemo barua hiyo ya kufutwa kazi.
Amesema sababu zilizowasilishwa katika pingamizi la upande wa uetezi za kutaka barua hiyo isipokelewe mahakamani kama kielelezo hazina msingi hivyo zimekataliwa na barua imepokelewa kama kielelezo Namba 6. Amesema shahidi ndiyo mtu sahihi anayepaswa kuwasilisha kielelezo hiki mahakamani kwani yeye ndie anayetunza mafaili yote ya wafanyakazi wa Takukuru na kwamba alihusika katika suala la kujadiliwa nidhamu ya mshtakiwa Gugai.
Mbali na Gugai, washtakiwa wengine, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali.Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decemba 2015.
Inadaiwa akiwa jijini Dar es Salaam kama mwajiriwa wa TAKUKURU alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh 3.6 bilioni ambazo hazilingani na kipato chake cha awali na cha sasa cha zaidi ya Tsh.milioni 800,huku akishindwa kuzitolea maelezo.
Hivyo makala MAHAKAMA YAPOKEA BARUA YA KUFUTWA KAZI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU
yaani makala yote MAHAKAMA YAPOKEA BARUA YA KUFUTWA KAZI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAPOKEA BARUA YA KUFUTWA KAZI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/mahakama-yapokea-barua-ya-kufutwa-kazi.html
0 Response to "MAHAKAMA YAPOKEA BARUA YA KUFUTWA KAZI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU"
Post a Comment