Loading...
title : MARUFUKU BUTURA NA BIASHARA YA MAGENDO KATIKA KAHAWA-DKT TIZEBA
link : MARUFUKU BUTURA NA BIASHARA YA MAGENDO KATIKA KAHAWA-DKT TIZEBA
MARUFUKU BUTURA NA BIASHARA YA MAGENDO KATIKA KAHAWA-DKT TIZEBA
Na Mathias Canal-WK, Kagera
Biashara ya kuuza Kahawa nje ya nchi pasina kufuata utaratibu wa kisheria (magendo) imepigwa marufuku hivyo atakayebainika kuendelea na biashara hiyo atachukuliwa hatua Kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Agizo hilo limehusisha pia zuio la wananchi kuuza kahawa mbichi ingali bado shambani haijakomaa (Butula) kwani kufanya hivyo ni kudhoofisha na kuzorotesha juhudi za muda mrefu alizotumia mkulima wa kahawa na kumkosesha mapato stahiki.
Marufuku hiyo imetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba Leo 10 Julai 2018 wakati akizungumza na wadau wa zao la kahawa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa.
Waziri Tizeba alisema kuwa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ambayo ndio mkataba wa wananchi na serikali yao inatoa maelekezo ya kuwezesha upatikanaji wa Masoko ya Mazao ya Kilimo kwa kuviimarisha na kuviwezesha vyama vya ushirika kuwa na uwezo wa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ya ndani na nje kwa kuweka mfumo madhubuti wa ukusanyaji, uchambuzi na uenezaji wa taarifa za Masoko na kutoa elimu juu ya uongezaji thamani na biashara.
Alisema serikali itajitahidi kutafuta bei nzuri ya zao la kahawa ndani na nje ya Afrika Mashariki ili wananchi wapate faida na tija ya Kilimo huku akieleza kuwa wakulima wa kahawa kote nchini hawawezi kuona mafanikio ya Kilimo hicho kwa kuendeleza biashara ya magendo sambamba na biashara ya kahawa mbichi ikiwa shambani (Butura).
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akieleza maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi wakati akizungumza na wadau wa zao la kahawa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Wadau wa zao la kahawa wakifatilia kwa makini mkutano uliowakutanisha wadau wa zao hilo uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa zao la kahawa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018. Wengine pichani kulia ni waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Mhe Salum Kijuu.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Tizeba wakikagua na kuzungumza na viongozi wa Chama Cha Msingi cha Karukwanzi Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018.
Hivyo makala MARUFUKU BUTURA NA BIASHARA YA MAGENDO KATIKA KAHAWA-DKT TIZEBA
yaani makala yote MARUFUKU BUTURA NA BIASHARA YA MAGENDO KATIKA KAHAWA-DKT TIZEBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MARUFUKU BUTURA NA BIASHARA YA MAGENDO KATIKA KAHAWA-DKT TIZEBA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/marufuku-butura-na-biashara-ya-magendo_10.html
0 Response to "MARUFUKU BUTURA NA BIASHARA YA MAGENDO KATIKA KAHAWA-DKT TIZEBA"
Post a Comment