Loading...
title : MKOA WA GEITA KUFANYA MAPINDUZI YA MADINI YA DHAHABU NA VITO
link : MKOA WA GEITA KUFANYA MAPINDUZI YA MADINI YA DHAHABU NA VITO
MKOA WA GEITA KUFANYA MAPINDUZI YA MADINI YA DHAHABU NA VITO
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MKOA wa Geita unatarajia kufanya mapinduzi katika sekta ya madini ya Dhahabu na Vito katika kuunga mkono juhudi za Serikali yenye dhamira ya uchumi wa viwanda.
Mapinduzi hayo yatapatikana kupitia maonesho ya kwanza ya madini ya dhahabu yanayotarajiwa kufanyika Septemba 25 hadi 29 mwaka huu mkoani humo yakiwa na lengo la kuonesha jinsi dhahabu inavyopatikana na kuondoa imani potofu kuwa hupatikana kwa kuweka dawa.
Maonesho hayo yameratibiwa kupitia Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade) ambao ndio watakaotoa wataalam na vifaa kwa ajili ya kufanikisha maonesho hayo.
Akizungumza leo Mkuu wa Mkoa wa Geita,Robert Gabriel amesema hayo katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ( DITF) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Barbara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Amesema Maonesho ya dhahabu yataleta tija kwa wachimbaji wadogo kwa kupata teknolojia na hata kwa Taifa kwa kuwa yataongeza wigo wa upatikanaji wa mapato na hata kuongeza uzalishaji wa madini hayo nchini.
Amesema kwa sasa kumekuwa na uchimbaji holela kwa wachimbaji wadogo wadogo na maonesho hayo yatasaidia kupata teknolojia mpya na za kisasa kuhusu sekta hiyo namna bora ya udhibiti wa madini na hats kuhakikisha dhahabu ipagokanayo inanufaisha Watanzania.
Gabriel amesema katika maonesho hayo kutakuwa na mwanya wa kupima udongo na hata utafiti wa kijiolojia ili kuweza kujua udongo upi wenye dhahabu na ambao hauna.
Amesema asilimia Tanzania imejaliwa kuwa na madini ya Vito vya thamani na asilimia 35 ya Vito vinavyotengenezwa hutokana na dhahabu kutoka Geita.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tantrade Edwin Rutageruka amesema Mamlaka hiyo itatoa wataalam wanne kwa ajili ya kuwezesha maonesho hayo na baadhi ya vifaa vitapelekwa Geita ambavyo vinayumikabkatika Maonesho haya ya DITF.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana maonesho ya Madini ya Dhahabu na Vito yatakayofanyika Septemba 25 hadi 29 katika Mkoa huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade, Edwin Rutageruka akizungumza kuhusiana na wataalam wa Tantrade kushirikiana na Sekretarieti ya Mkoa wa Geita katika kuandaa maonesho hayo.
Hivyo makala MKOA WA GEITA KUFANYA MAPINDUZI YA MADINI YA DHAHABU NA VITO
yaani makala yote MKOA WA GEITA KUFANYA MAPINDUZI YA MADINI YA DHAHABU NA VITO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKOA WA GEITA KUFANYA MAPINDUZI YA MADINI YA DHAHABU NA VITO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/mkoa-wa-geita-kufanya-mapinduzi-ya.html
0 Response to "MKOA WA GEITA KUFANYA MAPINDUZI YA MADINI YA DHAHABU NA VITO"
Post a Comment