Loading...
title : WAKAZI KIGAMBONI WAMWANGUKIA RAIS MAGUFULI,RC MAKONDA KUWASAIDIA KUTATUA KERO INAYOWAKABILI
link : WAKAZI KIGAMBONI WAMWANGUKIA RAIS MAGUFULI,RC MAKONDA KUWASAIDIA KUTATUA KERO INAYOWAKABILI
WAKAZI KIGAMBONI WAMWANGUKIA RAIS MAGUFULI,RC MAKONDA KUWASAIDIA KUTATUA KERO INAYOWAKABILI
WAKAZI wa Kata ya Somangila wilayani Kigamboni mkoani Dar es Salaam wamemuomba Rais Dk.John Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es SalaamPaul Magufuli kuingilia kati suala la mgogoro uliopo kwenye Kata hiyo uliokwamisha miundombinu ya barabara kusimama.
Hayo yamebainishwa jana na wakazi wa eneo hilo wakati wakizungumza na waandishi wa habari walipokuwa wamekutana na Diwani wa Kata hiyo,Chichi Masanja na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo Sadick Mohamed ambapo wameelezea kuhusu kero yao ya miundombinu ya barabara ambayo imekwamishwa na mmoja wa Mkurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam.
Wakazi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti wameelezea kwamba Mkurugenzi huyo(wakamtaja ) amezungushia uzio kwenye eneo la barabara hivyo kusababisha usumbufu hasa kwa akina mama wajawazito wanapohitaji kwenda kujifungua.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo kijiji cha Dege Kata ya Somangila, Sadick Mohamed, amesema kuwa Mkurugenzi huyo amejimilikisha zaidi ya ekari 100 ambazo haziendelezwi na hivyo zimesababisha kuwepo kwa wahalifu wanaojificha kwenye vichaka vilivyopo kwenye mashamba hayo.
Amesema kuwa mbali na wahalifu pia amekwamisha miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa Barabara unaosimamiwa na Wakala wa Barabara vijijini na mijini (TARULA) ambayo tayari fedha zake zilikwisha tengwa katika bajeti ya 2017/18 hivyo ujenzi huo ukiendelea kusimama fadha hizo zinaweza kurudi Serikali kuu.
Wakati huo huo Diwani wa Kata hiyo Chichi Masanja amesema ni vema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuingila kati suala hilo kwani linakwamisha maendeleo katika wilaya hiyo.Na iwapo ipo haja ya Rais Magufuli kuingilia kati utakuwa jambo jema zaidi.
Hivyo makala WAKAZI KIGAMBONI WAMWANGUKIA RAIS MAGUFULI,RC MAKONDA KUWASAIDIA KUTATUA KERO INAYOWAKABILI
yaani makala yote WAKAZI KIGAMBONI WAMWANGUKIA RAIS MAGUFULI,RC MAKONDA KUWASAIDIA KUTATUA KERO INAYOWAKABILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKAZI KIGAMBONI WAMWANGUKIA RAIS MAGUFULI,RC MAKONDA KUWASAIDIA KUTATUA KERO INAYOWAKABILI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/wakazi-kigamboni-wamwangukia-rais.html
0 Response to "WAKAZI KIGAMBONI WAMWANGUKIA RAIS MAGUFULI,RC MAKONDA KUWASAIDIA KUTATUA KERO INAYOWAKABILI"
Post a Comment