Loading...

MPINA AUNDA KANDA MPYA YA ULINZI NA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI ZIWA VICTORIA

Loading...
MPINA AUNDA KANDA MPYA YA ULINZI NA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI ZIWA VICTORIA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MPINA AUNDA KANDA MPYA YA ULINZI NA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI ZIWA VICTORIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MPINA AUNDA KANDA MPYA YA ULINZI NA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI ZIWA VICTORIA
link : MPINA AUNDA KANDA MPYA YA ULINZI NA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI ZIWA VICTORIA

soma pia


MPINA AUNDA KANDA MPYA YA ULINZI NA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI ZIWA VICTORIA

NA JOHN MAPEPELE,DODOMA

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameunda Kanda mpya ya Ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Ziwa Victoria na kuteua maafisa wapya wataokuwa na jukumu la kudhibiti na kutokomeza uvuvi haramu na biashara haramu ya mazao ya uvuvi katika Ziwa Victoria ifikapo Desemba 2018.

Akizungumza jijini Dodoma mwishoni mwa wiki, Waziri Mpina amemteua Didas Mtambalike kuwa Mkuu mpya wa Kanda mpya ya Ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Ziwa Victoria huku akiunda kanda mbili za kiulinzi za Sengerema na Ukerewe .Pia Serikali imeanzisha Kituo cha Ukaguzi wa Mazao ya Uvuvi mkoani Singida na kuweka vizuizi katika maeneo yote yaliyoripotiwa kuwepo matukio ya utoroshaji wa rasilimali za uvuvi hapa nchini.

Maafisa wengine walioteuliwa na Waziri Mpina kuongoza kanda zingine ni pamoja na West Mbembati ambaye ataongoza Kanda ya Kagera, Vicenti Masui Munda Kanda ya Mwanza, Jairos Mahenge Kanda ya Mkoa wa Mara.Wengine ni Judith Mgaya atakayeongoza Kanda ya Kiulinzi Ukerewe na Roman Mkenda Kanda ya Mkoa wa Geita, Wencleslaus Luhasile aliyekuwa Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Magu sasa ataongoza Kanda ya Kiulinzi ya Sengerema na Samson Mboje kutoka Kituo cha Usimamizi na Ulinzi wa Rasilimali Kanda ya Mwanza, sasa ameteuliwa kuongoza Kanda ya Simiyu/Magu.

Aidha Waziri Mpina alisisitiza kuwa katika operesheni inayoendelea Serikali inaandaa utaratibu wa kwenda na mahakama inayotembea ili watuhumiwa na wahalifu wahukumiwe pale pale wakiwa na mashahidi wao.Kuhusu maendeleo ya wavuvi wadogo, Waziri Mpina amesema Wizara yake kwa kushirikiana na Benki ya NMB inawafuatilia wavuvi na kuwafungulia akaunti ambapo hadi sasa zaidi ya wavuvi 20,000 wamefikiwa.
Picha ya pamoja ya Maafisa (waliosimama) walioteuliwa kusimamia rasilimali za uvuvi katika kanda maalumu kwenye Ziwa Victoria na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina mwenye koti jeupe kushoto kwake ni Mahamoud Mgimwa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji kulia ni Katibu Mkuu Uvuvi Rashid Tamatama na Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Magesa Bulayi.




Hivyo makala MPINA AUNDA KANDA MPYA YA ULINZI NA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI ZIWA VICTORIA

yaani makala yote MPINA AUNDA KANDA MPYA YA ULINZI NA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI ZIWA VICTORIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MPINA AUNDA KANDA MPYA YA ULINZI NA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI ZIWA VICTORIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/mpina-aunda-kanda-mpya-ya-ulinzi-na_24.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MPINA AUNDA KANDA MPYA YA ULINZI NA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI ZIWA VICTORIA"

Post a Comment

Loading...