Loading...

Naibu Katibu Mkuu ataka vikwazo vya lugha kuondolewa kwenye mitaala Afrika

Loading...
Naibu Katibu Mkuu ataka vikwazo vya lugha kuondolewa kwenye mitaala Afrika - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Naibu Katibu Mkuu ataka vikwazo vya lugha kuondolewa kwenye mitaala Afrika, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Naibu Katibu Mkuu ataka vikwazo vya lugha kuondolewa kwenye mitaala Afrika
link : Naibu Katibu Mkuu ataka vikwazo vya lugha kuondolewa kwenye mitaala Afrika

soma pia


Naibu Katibu Mkuu ataka vikwazo vya lugha kuondolewa kwenye mitaala Afrika

Na Mwandishi wetu
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Elimu ya Ufundi, Avemaria Semakafu ametaka kuvunjwa kwa vikwazo vya lugha vinavyosababisha mkanganyiko wa utoaji elimu barani Afrika kwa kutumia Kiswahili.

Alisema mataifa ya Afrika yamekuwa yakibabaika katika matumizi ya lugha za kikoloni ambazo zimesababisha pia kuwa na ulingafu dhaifu wa utoaji elimu kwa bara hili.

Alisema hayo kwenye kongamano la Mataifa zaidi ya 16 yaliyo Kusini mwa Jangwa la Sahara ambayo yamekuwa yakikutana kuanzia Jumatano kujadiliana namna bora ya kutengeneza mitaala na vifaa vya kufundishia ili kuboresha mbinu za kufundisha na kujifunza.

Alisema ipo haja ya kuondokana na mifumo ya mapokeo ambayo imejaa taratibu za kikoloni zinazompima mtu kwa mitihani na akifeli kuonekana hana uwezo, wakati waliofeli ndio wanafanya vyema katika maisha ya kawaida ya kila siku.

Akizungumza na wawakilishi hao ambao wanashiriki katika kongamano la siku tatu katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Kinondoni Dar Es Salaam, Naibu Katibu Mkuu huyo alisema ipo haja ya kuangalia mfumo mzima na kupata vigezo halali vya kutathmini mafanikio ya elimu kwa kuangalia elimu yenyewe mitaala na namna ya uwekaji wa ulinganifu wa matokeo.

Alitaka mataifa ya Afrika kutumia lugha moja ya Kiswahili katika ufundishaji ili kuondokana na kikwazo cha lugha ambacho alisema ni moja ya kifaa cha utamaduni wa utoaji elimu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Elimu ya Ufundi, Dk . Avemaria Semakafu akifungua kongamano la kikanda kuhusu ulinganifu wa mafunzo, mitaala, mafunzo kwa walimu na vifaa vya kufundishia mataifa zaidi ya 16 yaliyo Kusini mwa Jangwa la Sahara ili kubadilishana uzoefu wa namna ya kushirikiana na kufanyakazi kimtandao ili kuboresha mazingira ya kujifunza kwa mamilioni ya wanafunzi kwenye nchi hizo liliofanyika jijini Dar es Salaam. Kongamano hili limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni-UNESCO na linaendeshwa na mtandao wa TALENT.
Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki na Afisa Mwakilishi wa Unesco nchini, Ann Therese Ndong- Jatta akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo wakati wa kongamano la kikanda kuhusu ulinganifu wa mafunzo, mitaala, mafunzo kwa walimu na vifaa vya kufundishia lililokutanisha nchi 16 ili kutekeleza moja ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs, lengo la nne lililofanyika Jijini Dar es Salaam. Kongamano hili limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na linaendeshwa na mtandao wa TALENT.
Mratibu wa mtandao wa watoa elimu na mafunzo kwa mabadiliko (TALENT) kutoka UNESCO Dakar, Valérie Djioze-Gallet akizungumzia madhumuni kuratibu kongamano hilo la kikanda linalojadili kuhusu ulinganifu wa mafunzo, mitaala, mafunzo kwa walimu na vifaa vya kufundishia ili kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu hasa kwenye nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA) ili kufikia lengo la nne la maendeleo endelevu (SDGs) katika elimu. Kongamano hili limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na linaendeshwa na mtandao wa TALENT.

Baadhi ya wadau kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia mada kwenye kongamano la kikanda linalohusu ulinganifu wa mafunzo, mitaala, mafunzo kwa walimu na vifaa vya kufundishia ili kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu hasa kwenye nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA).
Baadhi ya wanakamati ya maandalizi ya kongamano hilo kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Elimu ya Ufundi, Dk . Avemaria Semakafu katika picha ya pamoja ya washiriki wa kongamano la kikanda kuhusu ulinganifu wa mafunzo, mitaala, mafunzo kwa walimu na vifaa vya kufundishia mataifa zaidi ya 16 yaliyo Kusini mwa Jangwa la Sahara ili kubadilishana uzoefu wa namna ya kushirikiana na kufanyakazi kimtandao ili kuboresha mazingira ya kujifunza kwa mamilioni ya wanafunzi kwenye nchi hizo liliofanyika jijini Dar es Salaam. Kongamano hili limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni-UNESCO na linaendeshwa na mtandao wa TALENT.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Naibu Katibu Mkuu ataka vikwazo vya lugha kuondolewa kwenye mitaala Afrika

yaani makala yote Naibu Katibu Mkuu ataka vikwazo vya lugha kuondolewa kwenye mitaala Afrika Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Katibu Mkuu ataka vikwazo vya lugha kuondolewa kwenye mitaala Afrika mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/naibu-katibu-mkuu-ataka-vikwazo-vya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Naibu Katibu Mkuu ataka vikwazo vya lugha kuondolewa kwenye mitaala Afrika"

Post a Comment

Loading...