Loading...
title : Halmashauri ya Bagamoyo yajadili majibu ya hoja mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali
link : Halmashauri ya Bagamoyo yajadili majibu ya hoja mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali
Halmashauri ya Bagamoyo yajadili majibu ya hoja mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali
MKAGUZI wa ndani wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Bw. Paschal Shindai ameisihi taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) na Jeshi la polisi kuwasilisha nyaraka za malipo ambazo amesema zipo mikononi mwao kwa miaka 10 sasa ili waweze kufunga hoja.
Aidha ameweka bayana kwamba kati ya hoja 79 zilizokuwepo katika halmashauri hiyo, hoja 62 zilipata majibu ya kuridhisha na kufungwa ambapo 17 hazijafungwa hadi sasa
Bw . Shindai aliyasema hayo katika kikao maalum kilicholenga kupokea na kujadili majibu ya hoja mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG)mwaka 2016/2017kilichowashirikisha madiwani, katibu tawala wa mkoa wa Pwani (RAS) na mkaguzi mkuu wa nje wa mkoa.
Bw. Shindai alisema katika ukaguzi maalum uliofanyika mwaka wa fedha 2008/2009 imebainika hati za malipo zenye thamani ya milioni 158.347.155 hazikupatikana kukamilisha zoezi la ukaguzi na kwamba hati zote za malipo ambazo hazijapatikana kwa ajili ya ukaguzi maalum zilikuwa kwenye vyombo vya upelelezi vya TAKUKURU na jeshi la polisi .
Alisema ofisi yake imeshachukua hatua ya kuandika barua za kuomba taasisi hizo ziwasilishe nyaraka hizo za malipo kwa ajili ya ukaguzi lakini hazijawasilishwa na kusababisha hoja kushindwa kufungwa.
Kamati ya ukaguzi iliitaka menejimenti ifuatilie nyaraka hizo na kama kuna sababu za kutopewa nyaraka hizo basi TAKUKURU itoe kwa maandishi.Kwa upande wake, kamati ya fedha imeunga mkono maamuzi ya maoni hayo ya kamati ya ukaguzi.
Pamoja na hayo Bw. Shindai alielezea pia kuna hati za malipo zenye thamani ya zaidi ya milioni 92.935 kwa mwaka 2008/2009 kipindi cha ukaguzi maalum hazikupatikana na hazijakaguliwa . Hata hivyo amesema kuna kesi na mashauri mbalimbali yaliyoko mahakamani na hadi kufikia mwaka wa fedha 2012/2013 halmashauri ilikuwa bado ina mashauri 33 mahakamani .
"Katika ufuatiliaji wa hoja kwa miaka ya nyuma mwaka wa fedha 2008/2009,2010/2011,2012/2013,2013/2014 na mwaka 2015/2016 hoja 17 hazijafungwa.
"Hoja za ukaguzi kwa mwaka husika yaani mwaka wa fedha 2016/2017 hoja 20 kati ya hizo tisa zimefungwa na 11 hazijafungwa", alisisitiza Bw. Shindai. Katibu tawala wa mkoa wa Pwani Bw. Zuberi Samataba alisema atawasiliana na kamanda wa TAKUKURU mkoa Suzan Raymond na jeshi la polisi ili kuangalia namna ya kupata nyaraka ama taarifa za kimaandishi ili hoja ziweze kufungwa . Aliipongeza halmashauri hiyo kwa kupata hati safi mwaka huu .
" Kuweni makini wakati wa kuandaa taarifa za mahesabu. Shirikianeni na muwe kitu kimoja baina ya wataalmu,watendaji,mkurugenzi na madiwani "alisema Bw. Samataba.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Bagamoyo, Fatuma Latu alipokea ushauri na maelekezo waliyopatiwa na kudai watayafanyia kazi .
Kikao maalum kilicholenga kupokea na kujadili majibu ya hoja mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG)mwaka 2016/2017 kilichowashirikisha madiwani wa Bagamaoyo na mkaguzi mkuu wa nje wa mkoa
Mkaguzi wa ndani wa halmashauri ya Bagamoyo Bw. Paschal Shindai akizungumza katika kikao maalum cha kujadili majibu ya hoja mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG)mwaka 2016/2017,kilichowashirikisha madiwani, katibu tawala wa mkoa wa Pwani (RAS) na mkaguzi mkuu wa nje wa mkoa.
Katibu tawala wa mkoa wa Pwani Zuberi Samataba akizungumza jambo katika kikao maalum kilicholenga kupokea na kujadili majibu ya hoja mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG)mwaka 2016/2017,kilichowashirikisha madiwani wa Bagamaoyo na mkaguzi mkuu wa nje wa mkoa. Habari na picha na Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Hivyo makala Halmashauri ya Bagamoyo yajadili majibu ya hoja mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali
yaani makala yote Halmashauri ya Bagamoyo yajadili majibu ya hoja mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Halmashauri ya Bagamoyo yajadili majibu ya hoja mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/halmashauri-ya-bagamoyo-yajadili-majibu.html
0 Response to "Halmashauri ya Bagamoyo yajadili majibu ya hoja mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali"
Post a Comment