Loading...

NAIBU WAZIRI ATEMBELEA VIWANDA VYA NGOZI KILIMANJARO

Loading...
NAIBU WAZIRI ATEMBELEA VIWANDA VYA NGOZI KILIMANJARO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAIBU WAZIRI ATEMBELEA VIWANDA VYA NGOZI KILIMANJARO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAIBU WAZIRI ATEMBELEA VIWANDA VYA NGOZI KILIMANJARO
link : NAIBU WAZIRI ATEMBELEA VIWANDA VYA NGOZI KILIMANJARO

soma pia


NAIBU WAZIRI ATEMBELEA VIWANDA VYA NGOZI KILIMANJARO


Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvu vi Mhe.Abdalla Hamisi Ullega amefanya ziara Mkoani Kilimanjiro na kutembele jumla ya Viwanda vya ngozi vitatu na wadau wengine wa Sekta ya Mifugo.

Mmiliki wa Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi cha Himo Tanners & Planters LTD Bw.Waiso amemweleza Naibu Waziri kuwa changamoto kuwa iliyopo kwa sasa katika kiwanda hicho ni pamoja na tozo nyingi zisizo na tija ambazo zinatozwa kuanzia Serikali ya kijiji mpaka Serikali Kuu.

"Tozo zimekuwa nyingi mno katika  Viwanda,ambapo inafikia wakati kiwanda kinashindwa kujiendesha kwa Ufanisi kwa sababu ya Muda na gharama za kufuatilia tozo hizo katika mamlaka Husika"Alisema Waiso.

Aidha Waiso alitaja baadhi ya Tozo hizo kuwa ni pamoja na Service Levy,Export Permit,Business Licence,Water use fee,Water right fee na Chemical Permit fee.

Pia Mhe Ulega alipata fursa ya kutembele kituo cha Utafiti wa Mifugo, West Kilimanjaro (TALIRI), kiwanda cha kusindika ngozi cha  Moshi Leather industries limited,Shamba la mifugo Kafoi,Watengenezaji wa chakula cha Mifugo, Marenga Millers Company LTD na kushuhudia uwekezaji mkubwa wa Shamba la Kuzalisha Kuku wazazi la The Irvines Group katika Halmashauri ya Siha.

Shamba la Irvines hapa Tanzania Lipo katika Mikoa ya Kilimanjaro katika Halmashauri ya Siha,Pwani na Dar es salaam.Mpaka sasa Irvines hapa Tanzania kwa mwaka inatotolesha Vifaranga 13 M, na kama soko litaruhusu shamba hilo linauwezo wa kutotolesha Vifaranga zaidi 25 M kwa mwaka

Shamba la Irvines Group linazalisha na kutotolesha vifaranga Milioni 77 vya kuku wa nyama na Mayai katika nchi za Botswana,Zimbabwe na Msumbiji.

Mhe.Ulega akifanya majumuisho ya ziara yake katika Halmashauri ya siha na  kuongea na Wafugaji, Ulega amesema kuwa Viwanda karibu vyote vya ngozi vinafanya kazi nzuri isipokuwa kuna changamoto ndogondogo ambazo zinatakiwa  kufanyiwa kazi.

Awali Ulega akiongea na wafugaji wa Halmashauri ya Siha alisema kuwa Serikali ya  awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais John Joseph Pombe Magufuli inawajali wafugaji wake kwani tayari kwa Kupitia taasisi yake ya NARCO ipo katika mpango wa kuligawa kiasi cha Hekta Mia saba (700) eneo la NARCO ili liwekewe mpango bora wa matumizi, wakati wa kiangazi wafugaji waweze kupata malisho ya Mifugo yao  katika eneo hilo na kuchangia kiasi kidogo cha fedha ili kuweza kuimarisha miundombinu ya eneo husika.

"Serikali haiwezi kuvumilia kuona Mifugo inakufa kwa kukosa malisho wakati maeneo ya kulishia yapo,ndio maana ikaamua kuja na huu mpango ili kuokoa Rasilimali hii ya Taifa isipotee"Alisema Ulega.

Ulega alisisitiza tena kwa kusema"Wafugaji lazima tukubali sasa kufuga kisasa,Kwasababu ardhi haiongezeki,isipokuwa Mifugo Inaongezeka na watu wanazidi kuongezeka,hivyo hatuna budi kuwa na Mifugo michache lakini itakayotuletea tija"Alisema.

Ili tuweze kufikia Tanzania  ya Viwanda,tunahitaji Mifugo iliyonenepeshwa vizuri ili tuweze kupata nyama bora na soko la uhakika.

Naibu Waziri Ulega aliwaonya wafugaji hao kuwa mpango huo wa NARCO ukikamilika wa kuwakodisha maeneo ya kulishia Mifugo yao wakati wa kiangazi (ukame) Mfugaji yeyote atakayegundulika kuruhusu mifugo kutoka nchi jirani na kuingia nchini na kulisha malisho hayo,Serikali haita sita kusitisha mara Mpango huo.









Hivyo makala NAIBU WAZIRI ATEMBELEA VIWANDA VYA NGOZI KILIMANJARO

yaani makala yote NAIBU WAZIRI ATEMBELEA VIWANDA VYA NGOZI KILIMANJARO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI ATEMBELEA VIWANDA VYA NGOZI KILIMANJARO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/naibu-waziri-atembelea-viwanda-vya_20.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NAIBU WAZIRI ATEMBELEA VIWANDA VYA NGOZI KILIMANJARO"

Post a Comment

Loading...