Loading...
title : TRA YAWATAKA WENYE VIWANDA KUTOA TAKWIMU SAHIHI ZA UZALISHAJI WAO
link : TRA YAWATAKA WENYE VIWANDA KUTOA TAKWIMU SAHIHI ZA UZALISHAJI WAO
TRA YAWATAKA WENYE VIWANDA KUTOA TAKWIMU SAHIHI ZA UZALISHAJI WAO
Na Rachel Mkundai, Manyara
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara wenye viwanda vya kutengeneza mali ghafi za kutengenezea pombe kali kutoa tawimu sahihi ya kiasi kinachozalishwa na mahali inapouzwa ili serikali iweze kukusanya kodi yake stahiki kupitia pombe kali.
Hayo yamesemwa na Kamishna waKodi za Ndani wa TRA Bw Elijah Mwandumbya mara baada ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza sukari cha Manyara Sugar Company Limited kilichopo mkoani Manyara na kuongeza kuwa takwimu hizo zitawezesha TRA kufuatilia kwa karibu na kupata takwimu sahihi za kikodi na kuongeza makusanyo ya mapato.
“Tunafahamu kwamba “Molasis” au mali ghafi inayotokana na zao la miwa baada ya kutengeneza sukari ni bidhaa inayotumika kutengenezea pombe kali na hivyo takwimu zitatuwezesha kufuatilia wafanyabiashara wanaonunua bidhaa hiyo na kutengenezea pombe kali ili nasi tukadai kodi yetu na kodi hiyo ilete tija kwa taifa”, amesema Bw. Mwandumbya
Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (wa pili kulia) akiwa ameongozana na uongozi wa Kiwanda cha Manyara Sugar Company Limited kuelekea katika eneo la uzalishaji sukari wakati alipofanya ziara ya kikazi kusikiliza changamoto za Wafanyabiashara.
Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (katikati) akitoa maagizo kwa uongozi wa Kiwanda cha Manyara Sugar Company Limited kuhusu kutoa takwimu sahihi uzalishaji sukari wakati alipofanya ziara ya kikazi kusikiliza changamoto za Wafanyabiashara.
Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Kiwanda cha Manyara Sugar Company Limited, Bw. Pratap Sisudya wakati alipofanya ziara ya kikazi kusikiliza changamoto za Wafanyabiashara.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Manyara Sugar Company Limited, Bw. Pratap Sisudya (katikati) akimweleza Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (wa pili kulia) moja ya mtambo utumikao kuzalisha sukari wakati alipofanya ziara ya kikazi kusikiliza changamoto za Wafanyabiashara.
Hivyo makala TRA YAWATAKA WENYE VIWANDA KUTOA TAKWIMU SAHIHI ZA UZALISHAJI WAO
yaani makala yote TRA YAWATAKA WENYE VIWANDA KUTOA TAKWIMU SAHIHI ZA UZALISHAJI WAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TRA YAWATAKA WENYE VIWANDA KUTOA TAKWIMU SAHIHI ZA UZALISHAJI WAO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/tra-yawataka-wenye-viwanda-kutoa.html
0 Response to "TRA YAWATAKA WENYE VIWANDA KUTOA TAKWIMU SAHIHI ZA UZALISHAJI WAO"
Post a Comment