Loading...

NEW MILLENIUM WACHANGIA SH. MILIONI 4 MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO

Loading...
NEW MILLENIUM WACHANGIA SH. MILIONI 4 MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NEW MILLENIUM WACHANGIA SH. MILIONI 4 MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NEW MILLENIUM WACHANGIA SH. MILIONI 4 MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO
link : NEW MILLENIUM WACHANGIA SH. MILIONI 4 MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO

soma pia


NEW MILLENIUM WACHANGIA SH. MILIONI 4 MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO


MKE wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa amewaongoza wake wa viongozi kuchangia sh. milioni nne kwa ajili ya watoto wawili wanaohitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo.

“Kwa umoja wetu, na kwa kuguswa na uhitaji wa watoto wenye matatizo ya moyo, tuliamua tuchange fedha na zimefikia shilingi milioni nne ili tuweze kusaidia kuchangia gharama za matibabu kwa ajili ya watoto wawili,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Julai 27, 2018) wakati akizungumza na baadhi ya wazazi na watumishi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuwatembelea watoto wengine waliofanyiwa upasuaji wiki hii.

Mama Majaliwa ambaye aliongozana na wake wengine wa viongozi wakiongozwa na Mwenyekiti wa New Millenium Group, Mama Mbonimpaye Mpango, alikabidhi hundi kwa wazazi wa watoto wawili ambao ni Angela Francis (2) na Sabina Mnyango (4).

Watoto hao ni miongoni mwa watoto tisa wenye umri wa miezi mitatu hadi miaka 17 ambao walipangiwa kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na madaktari bingwa wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Chain of Hope la Uingereza. Matibabu hayo yalianza Julai 23, mwaka huu na yanatarajiwa kukamilishwa leo.

Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa akiwakabidhi hundi ya shilingi milioni nne wazazi wa watoto Anjela Francis (4) na Sabina Mnyango (4) fedha ambazo zimetolewa na kikundi cha wake wa viongozi cha New Millenium Group kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto hao ambao wanatibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Mhe. Mama Majaliwa pamoja na wake wa viongozi walipotembelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Chain of Hope ya nchini Uingereza. 
Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wake wa viongozi, wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na wazazi wa watoto ambao kikundi cha wake wa viongozi cha New Millenium Group kimewachangia shilingi milioni nne kwa ajili ya gharama za upasuaji wa moyo. Mhe. Mama Majaliwa pamoja na wake wa viongozi walipotembelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Chain of Hope ya nchini Uingereza. 
Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) aliyefanyiwa upasuaji wa kuziba matundu ya moyo katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Chain of Hope la nchini Uingereza. Mhe. Mama Majaliwa pamoja na wake wa viongozi wa kikundi cha Millennium Group walitembelea kambi hiyo leo na kuchangia shilingi milioni nne kwa ajili ya gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto wawili.




Hivyo makala NEW MILLENIUM WACHANGIA SH. MILIONI 4 MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO

yaani makala yote NEW MILLENIUM WACHANGIA SH. MILIONI 4 MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NEW MILLENIUM WACHANGIA SH. MILIONI 4 MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/new-millenium-wachangia-sh-milioni-4.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NEW MILLENIUM WACHANGIA SH. MILIONI 4 MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO"

Post a Comment

Loading...