Loading...
title : NSSF WATOA MSAADA WA ZAIDI YA MILIONI 4.5 MANISPAA YA IRINGA NA HALMASHAURI YA IRINGA
link : NSSF WATOA MSAADA WA ZAIDI YA MILIONI 4.5 MANISPAA YA IRINGA NA HALMASHAURI YA IRINGA
NSSF WATOA MSAADA WA ZAIDI YA MILIONI 4.5 MANISPAA YA IRINGA NA HALMASHAURI YA IRINGA
Na Francis Godwin, Michuzi Blog, Iringa
MFUKO wa hifadhi ya jamii (NSSF) umetoa msaada wa mashuka 300 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4.5 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na halmashauri ya Iringa mkoani Iringa kwa ajili ya kusaidia hospitali ,zahanati na vituo vya afya vyenye upungufu wa mashuka ya wagonjwa.
Akikabidhi msaada huo leo meneja wa NSSF mkoa wa Iringa Josephat Komba alisema kuwa NSSF imetoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maombi yaliyotolewa na Halmashauri hizo kwa NSSF kuomba kusaidiwa msaada wa mashuka.
Komba alisema kuwa NSSF kama mfuko wa hifadhi ya jamii unayojukumu la kuendelea kuunga mkono jitihada za Halmashauri nchini katika kutoa huduma za afya na pia unaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli kuona sekta ya afya inaendelea kuboreshwa zaidi.
Kwani alisema NSSF pamoja na majukumu mengine itaendelea kuwa karibu na jamii ya kitanzania kwani hatua ya waajiri kuwaunganisha wafanyakazi wao na NSSF ni kutaka kuona maisha yao yanaendelea kuboreshwa zaidi hivyo jukumu lao kuona NSSF inaendelea kuunga mkono azima ya serikali katika uboreshaji wa huduma za afya.
Meneja wa NSSF mkoa wa Iringa Josephat Komba(kushoto) akimkabidhi msaada wa shuka 200 kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Omary Mkangama kwa ajili ya Hospitali ya Frelimo
Wafanyakazi wa hospitali ya Frelimo wakitandika mashuka yaliyotolewa na NSSF
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa Robert Masunya (kulia ) akishukuru kwa msaada wa NSSF.
o
Meneja wa NSSF mkoa wa Iringa Josephat Komba (kushoto ) akimkabidhi msaada wa mashuka 100 mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa Robert Masunya. Picha na Francis Godwin, Michuzi Blog, Iringa
Hivyo makala NSSF WATOA MSAADA WA ZAIDI YA MILIONI 4.5 MANISPAA YA IRINGA NA HALMASHAURI YA IRINGA
yaani makala yote NSSF WATOA MSAADA WA ZAIDI YA MILIONI 4.5 MANISPAA YA IRINGA NA HALMASHAURI YA IRINGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NSSF WATOA MSAADA WA ZAIDI YA MILIONI 4.5 MANISPAA YA IRINGA NA HALMASHAURI YA IRINGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/nssf-watoa-msaada-wa-zaidi-ya-milioni.html
0 Response to "NSSF WATOA MSAADA WA ZAIDI YA MILIONI 4.5 MANISPAA YA IRINGA NA HALMASHAURI YA IRINGA"
Post a Comment