Loading...

OLENASHA:KINACHOTAKIWA KWA WANANCHI NI MAENDELEO NA SIYO SIASA CHAFU

Loading...
OLENASHA:KINACHOTAKIWA KWA WANANCHI NI MAENDELEO NA SIYO SIASA CHAFU - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa OLENASHA:KINACHOTAKIWA KWA WANANCHI NI MAENDELEO NA SIYO SIASA CHAFU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : OLENASHA:KINACHOTAKIWA KWA WANANCHI NI MAENDELEO NA SIYO SIASA CHAFU
link : OLENASHA:KINACHOTAKIWA KWA WANANCHI NI MAENDELEO NA SIYO SIASA CHAFU

soma pia


OLENASHA:KINACHOTAKIWA KWA WANANCHI NI MAENDELEO NA SIYO SIASA CHAFU


Na.Vero Ignatus Ngorongoro

Mbunge wa jimbo la Ngorongoro ambaye pia ni naibu waziri wa elimu sayansi na Teknolojia William Olenasha ameanza ziara ya kutembelea wananchi wa jimbo lake kwa ajili ya kueleza kazi aliyofanya kwa muda wa miaka mitatu tangu achaguliwe na wananchi wake ikiwemo mradi wa barabara ya Lami kutoka Loliondo mpaka Mto wa Mbu.

Imekuwa ni desturi ya mara kwa mara kwa mbunge huyo kutembelea wananchi wake kila kata ambapo kila kata amepita mara nne tangu achaguliwe kuwa muwakilishi wa wananchi Bungeni.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Ngaresero pamoja na kata ya Pinyinyi zilizopo katika wilaya hiyo Olenasha amesema kuwa yeye ni mbunge ambaye amechaguliwa na wananchi wanyonge ambao wana changamoto hivyo lazima azitatue kwa kuwa ndiyo jambo alilotumwa na wananchi kuwawakilisha.Amesema kwasasa serikali inayoongozwa na Raisi John Magufuli imejitofautisha sana na kipindi cha nyuma kwakuwa hata maeneo ambayo yalisahaulika kwa muda mrefu kwa sasa yameshaanza kupatiwa vipau mbele ikiwemo pia miradi mikubwa ambayo imepelekwa katika jimbo hilo la Ngorongoro.

Olenasha amesema kuwa tayari kupitia yeye kama mbunge wananchi wameshaanza kuletewa mradi mkubwa wa barabara ya lami ambao ni wa kihistoria kutoka Loliondo mpaka mto wa Mmbu kilomita 213 mradi ambao wengi walizani ni ndoto tayari umeshaanza kujengwa.“Napenda kuwataarifu wananchi kuwa ujenzi wa barabara ya lami umeshaanza na shilingi Bilioni 87 zimeshatolewa tayari jambo ambalo wengi walidhani ni ndoto lakini imewezekana na mradi umeanza kwa ksi kubwa”Alisema Olenasha

Hata hivyo Olenasha amemshukuru Raisi Dokta Magufuli kwa kuwapa kipau mbele katika kuletea wananchi wake maendeleo ambapo nje na mradi huo wa Barabara upo mradi wa Umeme,Afya,maji na Elimu ambapo miradi hiyo imeshaidhinishiwa fedha kwa ajili ya kuanza mara moja.Kwa upande wa wananchi ambao wameshiriki mkutano huo wa Mbunge wamesema kuwa tangu kuanza kwa historia ya Uhuru hawajawahi kupata mawasiliano hata ya Simu wala kuona kituo cha afya lakini kupitia mbunge wao wameona mafanikio hayo.

Pamoja na hayo wamesema kuwa mbunge wao amekuwa mstari wa mbele katika suala la maendeleo kwasababu kila mara anatembea jimboni kwake licha ya kuwa na changamoto zilizopo lakini wanampa ushirikiano mzuri ili afanikishe kile ambacho ameshakianza kwa muda mrefu.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Olenasha,ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Ngorongoro William Olenasha akizungumza na wananchi wa jimbo hilo.
Wananchi wa kijiji cha Ngarasero wakimsikiliza mbunge wao Wiliam Olenasha katika ziara yake ya kutembelea wananchi


Hivyo makala OLENASHA:KINACHOTAKIWA KWA WANANCHI NI MAENDELEO NA SIYO SIASA CHAFU

yaani makala yote OLENASHA:KINACHOTAKIWA KWA WANANCHI NI MAENDELEO NA SIYO SIASA CHAFU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala OLENASHA:KINACHOTAKIWA KWA WANANCHI NI MAENDELEO NA SIYO SIASA CHAFU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/olenashakinachotakiwa-kwa-wananchi-ni.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "OLENASHA:KINACHOTAKIWA KWA WANANCHI NI MAENDELEO NA SIYO SIASA CHAFU"

Post a Comment

Loading...