Loading...

RAIS MAGUFULI: WASIOPENDA UJIO WA NDEGE MPYA WATAPA TAABU SANA

Loading...
RAIS MAGUFULI: WASIOPENDA UJIO WA NDEGE MPYA WATAPA TAABU SANA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RAIS MAGUFULI: WASIOPENDA UJIO WA NDEGE MPYA WATAPA TAABU SANA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RAIS MAGUFULI: WASIOPENDA UJIO WA NDEGE MPYA WATAPA TAABU SANA
link : RAIS MAGUFULI: WASIOPENDA UJIO WA NDEGE MPYA WATAPA TAABU SANA

soma pia


RAIS MAGUFULI: WASIOPENDA UJIO WA NDEGE MPYA WATAPA TAABU SANA

*Asema anaamini Watanzania wengi wanatambua umuhimu wa ndege hiyo
*Asisitiza ujio wa ndege hizo zimenunuliwa kutokakana na kuziba mianya ya rushwa.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amesema ujio wa ndege mpya unafurahiwa na kila Mtanzania na kwamba yule ambaye haifurahii ajue atapa taabu sana huku akiwashukuru Watanzania wote kwa kufanikisha ujio wa ndege hizo.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati anazungumza kabla ya ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner ambapo amefafanua kuwa ujio wa ndege hizo unatokana na kutekeleza ahadi ya kufufua shirika la ndege nchini. Amesema katika juhudi hizo Serikali imeamua kununua ndege saba kwa fedha za Serikali na kwamba tayari ndege tatu zilishawasili nchini na leo ni ndege ya nne kuwasili nchini. 
“Mafanikio haya ni makubwa sana na niseme hajajileta yenyewe bali ni ya Watanzania wote.Nitumie nafasi hii kuwashukuru Watanzania wote na kubwa zaidi anawashukuru kwa kulipa kodi kwani ndio imesababisha kununuliwa kwa ndege hizo saba. “Hivyo niwashukuru wote ambao wameshiriki katika ujio wa ndege hizi.Ukweli Watanzania tukiamua tunaweza na niishukuru Kamati ya Miundombinu kwa kukubali kununuliwa kwa ndege hizi na kuunga mkono juhudi zinazoendelea,”amesema Rais Magufuli.

Ameongeza Serikali ya CCM iliamua kufufua shirika la ndege kuna sababu tatu , mowapo ni kurudhisha heshima ya Taifa kwani ilikuwa ni aibu kuwa nchi ambayo ina kila kitu halafu hakuna hata ndege ilikuwa ni aibu. “Tuliona tuanze kuitoa aibu hii ambayo tulikuwa tunaipata Watanzania.Kuna nchi ndogo lakini zina ndege lakini sisi hatukuwa nazo.Hivyo tuliona lazima tuiondoe aibu huu kwa kuwa na ndege.

“Watanzania wanahitaji usafiri wa ndege kwani mchango wake ni mkubwa na unahihitajika sana.Zipo sababu za watu kutopanda ndege ikiwamo ya kutokuwepo na miundombinu. “Sababu nyingine ya waanchi wengi kutopanda ndege ilikuwa ni gharama.Kwa watu wa Kagera wanafahamu kwenda Bukoba na kurudi ilikuwa ni Sh.milioni moja lakini sasa kupitia ndege za ATCL ni Sh.400,000,”amefafanua Rais.

Pia amesema sababu ya kufufua ATCL ni kukuza utalii kwani Tanzania inashika nafasi ya pili duniani huku akifafanua pamoja na kuwa na vivutio vya utalii idadi ya watalii ni ndogo. Amesema hiyo inatokana na kukosekana kwa ndege kwani kote ambako wanapokea idadi kubwa ya watalii inatokana na uwepo na ndege za uhakika katika nchi zao. Mnapokuwa na ndege watalii wengi wanakwenda kuangalia utalii wanatumia ndege , hivyo hata uamuzi wa ndege hii ni kutaka kubeba watalii wengi.

“Na ninaamini ndege hii itakapoanza kufanya kazi na ile nyingine itakapokuja itaongeza watalii,”amesema Rais Magufuli. Amesema amesikiliza maoni ya wananchi mbalimbali kutokana na ujio wa ndege hiyo ambapo wengi wameizungumzia vema na hivyo anwashukuru kwa ushirikiano wao. Pamoja na kuimarisha shirika la ndege ,Rais Magufuli amesema pia Serikali ya CCM inaendelea kuboresha usafiri wa majini , ujenzi wa miundombinu ya barabara yakiwamo madaraja na kwamba daraja linalojengwa Tazara litaitwa Mfugale. ia Rais Magufuli amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya nishati ya umeme, miundombinu ya afya na elimu na kufafanua anaamini ifikapo mwaka 2025 Watanzania watakuwa katika uchumi wa kati.

Rais Magufuli amesema maendeleo yanayopatikana sasa yanatokana na kuzima mianya ya rushwa na upotevu wa fedha kwani hivi sasa amebana upotevu wa fedha na matokeo yake fedha zinatumika katika kufanya maendeleo ya nchi.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege hiyo mpya na yakisasa aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali ikiwasili katika uwanja wa ndege wa wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


Hivyo makala RAIS MAGUFULI: WASIOPENDA UJIO WA NDEGE MPYA WATAPA TAABU SANA

yaani makala yote RAIS MAGUFULI: WASIOPENDA UJIO WA NDEGE MPYA WATAPA TAABU SANA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MAGUFULI: WASIOPENDA UJIO WA NDEGE MPYA WATAPA TAABU SANA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/rais-magufuli-wasiopenda-ujio-wa-ndege.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "RAIS MAGUFULI: WASIOPENDA UJIO WA NDEGE MPYA WATAPA TAABU SANA"

Post a Comment

Loading...