Loading...
title : RC MAKONDA AKABIDHI MWENGE WA UHURU KWA MKOA WA PWANI.
link : RC MAKONDA AKABIDHI MWENGE WA UHURU KWA MKOA WA PWANI.
RC MAKONDA AKABIDHI MWENGE WA UHURU KWA MKOA WA PWANI.
Mwamba wa habariMkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo July 12 amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo baada ya Mwenge huo kukamilisha shughuli ya uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 32.
RC Makonda amesema kuwa ndani ya siku tano ambazo mwenge ulikuwa jijini Dar es salaam umefanikiwa kutembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 36 ya maendeleo kwenye wilaya zote tano.
Aidha RC Makonda amewashukuru wananchi wa Dar es salaam kwa ushirikiano mkubwa walioonyesha tangu siku mwenge ulipoingia hadi leo alipoukabidhi kwa mkoa wa Pwani.
Hivyo makala RC MAKONDA AKABIDHI MWENGE WA UHURU KWA MKOA WA PWANI.
yaani makala yote RC MAKONDA AKABIDHI MWENGE WA UHURU KWA MKOA WA PWANI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA AKABIDHI MWENGE WA UHURU KWA MKOA WA PWANI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/rc-makonda-akabidhi-mwenge-wa-uhuru-kwa.html
0 Response to "RC MAKONDA AKABIDHI MWENGE WA UHURU KWA MKOA WA PWANI."
Post a Comment