Loading...
title : SERIKALI KUFUTA TOZO YA USAJILI,KUHUWISHA NA KUSHIKILIA USAJILI KWA WAWEKEZAJI WA NDANI
link : SERIKALI KUFUTA TOZO YA USAJILI,KUHUWISHA NA KUSHIKILIA USAJILI KWA WAWEKEZAJI WA NDANI
SERIKALI KUFUTA TOZO YA USAJILI,KUHUWISHA NA KUSHIKILIA USAJILI KWA WAWEKEZAJI WA NDANI
NA WAMJW-MWANZA
SERIKALI kupitia wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imefuta tozo ya usajili , kuhuwisha pamoja na kushikilia usajili wa bidhaa zao kwa wawekezaji wa ndani kupitia Mamlaka ya chakula na Dawa TFDA .
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,J insia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipotembelea kuangalia ujenzi wa jengo la TFDA ambalo linajengwsa Jijini Mwanza ili kusogeza huduma kwa wananchi wa mkoa huo.
“Ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kukuza nchi kupitia uchumi wa viwanda hivyo TFDA msiwe kikwazo kwa wawekezaji hao hivyo kuanzia leo nafuta tozo za kusajili bidhaa,kuhuwisha bidhaa na tozo ya kushikilia usajili wa bidhaa”, alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa kuendana na juhudi hizo pia Serikali imefuta tozo ya udhibiti ya thamani ya 0.25 za dawa,vifaa na vifaa tiba zinazoingizwa kwenye hospitali za Umma kutoka kwa wafadhili.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa TFDA ina wajibu wa kusimamia Tanzania isiwe jalala la bidhaa zisizo na ubora kwa watanzania hivyo wanatakiwa kuweka afya ya wananchi mbele kuliko manufaa binafsi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi. Agness Kijo amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo ukikamilika utasaidia kuhudumia huduma za kimaabara kwa bidhaa zinazoingia nchini kwani itakuwa sio lazima tena kwenda kupima bidhaa hizo jijini Dar es salaam.
Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kushoto wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la Mamlaka hiyo jijini Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi wa Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya afya Dkt. Mohammed Mohammed.
Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akipata maelezo juu ya sukari zinazopimwa ubora wake kutoka kwa Mkuu wa Maabara wa TFDA Kanda ya Ziwa Bw. Salum Kindoli wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la Mamlaka hiyo jijini Mwanza.
Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akipata baadhi ya maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya afya Dkt. Mohammed Mohammed kushoto wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la Mamlaka hiyo jijini Mwanza.
Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akikagua shughuli za ujenzi wa jengo la wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo hilo jijini Mwanza.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala SERIKALI KUFUTA TOZO YA USAJILI,KUHUWISHA NA KUSHIKILIA USAJILI KWA WAWEKEZAJI WA NDANI
yaani makala yote SERIKALI KUFUTA TOZO YA USAJILI,KUHUWISHA NA KUSHIKILIA USAJILI KWA WAWEKEZAJI WA NDANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUFUTA TOZO YA USAJILI,KUHUWISHA NA KUSHIKILIA USAJILI KWA WAWEKEZAJI WA NDANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/serikali-kufuta-tozo-ya.html
0 Response to "SERIKALI KUFUTA TOZO YA USAJILI,KUHUWISHA NA KUSHIKILIA USAJILI KWA WAWEKEZAJI WA NDANI"
Post a Comment