Loading...
title : Serikali yaendelea kuweka msukumo wa kukuza Sekta ya Filamu Nchini
link : Serikali yaendelea kuweka msukumo wa kukuza Sekta ya Filamu Nchini
Serikali yaendelea kuweka msukumo wa kukuza Sekta ya Filamu Nchini
Na Lorietha Laurence-WHUSM, Manyara.
Serikali imendelea kuweka msukumo wa kukuza Sekta ya filamu nchini,kwa kuendeleza utafiti, ubunifu na teknolojia ikiwemo kujenga mazingira wezeshi kwa wadau wake ili kuleta matokea chanya katika tasnia hiyo .
Hayo yamesemwa Mkoani Manyara na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wadau wa filamu katika Mkoa huo yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini.
Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa Mkoa wa Manyara una mazingira mazuri yenye fursa ya kuandaa filamu nzuri zenye ubora na uhalisia wa vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika Mkoa huo.
“Watu wa Manyara tumieni fursa hii nzuri mliyoipata katika mafunzo haya ambayo yanatolewa bure kwa kutengeneza filamu nzuri, ukizingatia mazingira yenu yana uhalisia mzuri wa kuvutia” amesema Dkt, Mwakyembe.
Aidha alizidi kufafanua kuwa kuna mambo mengi ya kuweka katika filamu, ikiwemo tamaduni zinazopatikana katika Mkoa wa Manyara, milima pamoja na uoto wa asili kitu kitakacholeta hali ya utofauti na wa kipekee .
Naye Kaimu Katibu Tawala kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw. Misaile Musa alizidi kuwasisitiza washiriki wa mafunzo hayo kujifunza kwa makini ili kuleta mabadiliko kwa kutengeneza filamu bora zenye viwango.
Kwa Upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini. Bibi. Joyce Fissoo amesema lengo la mafunzo hayo ni kuleta mabadiliko katika tasnia ya filamu nchini, ili kuwa na waandaji bora wa filamu.
Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na wadau wa filamu (hawapo katika picha) wakati wa kufungua mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wadau wa filamu leo katika Mkoa wa Manyara.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bw. Misaile Musa (kushoto) akiongea jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wadau wa Filamu wa Mkoa huo, ambayo yameandaliwa na Bodi ya Filamu nchini kulia ni Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bibi. Joyce Fissoo akiwasilisha mada kuhusu wajibu na majukumu ya Bodi ya Filamu katika kukuza sekta ya filamu , leo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta hiyo wa Mkoa wa Manyara.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Multi Choice nchini Bw. Johnstone Mshana akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu leo Mkoani Manyara.
Wadau wa sekta ya filamu wa Mkoa wa Manyara wakifuatilia uwasilishwaji wa mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini yenye lengo la kuwajengea uwezo wadau hao leo Mkoani humo. Picha na Lorietha Laurence-WHUSM.
Hivyo makala Serikali yaendelea kuweka msukumo wa kukuza Sekta ya Filamu Nchini
yaani makala yote Serikali yaendelea kuweka msukumo wa kukuza Sekta ya Filamu Nchini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali yaendelea kuweka msukumo wa kukuza Sekta ya Filamu Nchini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/serikali-yaendelea-kuweka-msukumo-wa.html
0 Response to "Serikali yaendelea kuweka msukumo wa kukuza Sekta ya Filamu Nchini"
Post a Comment