Loading...
title : Bilioni 45 kupeleka umeme kwa Vijiji 150 Morogoro
link : Bilioni 45 kupeleka umeme kwa Vijiji 150 Morogoro
Bilioni 45 kupeleka umeme kwa Vijiji 150 Morogoro
Na Veronica Simba – Kilosa
Imeelezwa kwamba, jumla ya shilingi bilioni 45 za kitanzania, zimetengwa na Serikali kwa ajili ya kupeleka umeme katika Vijiji 150 vya Mkoa wa Morogoro, kupitia Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza (REA IIIA.)
Hayo yamebainishwa Jumatatu, Julai 9, 2018 na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, wakati wa ziara yake katika Kijiji cha Mandela, Kata ya Magole, wilayani Kilosa; ambapo pamoja na mambo mengine, alizindua rasmi uwashaji wa umeme wa REA IIIA, kwa Mkoa wa Morogoro.
Akifafanua zaidi, Naibu Waziri alisema kuwa, miradi hiyo kwa ujumla wake, katika Awamu ya Kwanza inajumuisha Vijiji 3559 ambavyo vitatumia takribani shilingi bilioni 900 za kitanzania.
“Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais wetu John Magufuli, imejielekeza katika kuhakikisha nishati inafika kwenye maeneo mengi nchini ili kwenda kusukuma uchumi wa viwanda ambao tunaujenga,” alisema.
Akielezea hatua itakayofuata baada ya uzinduzi huo, Naibu Waziri alisema kuwa, ni kuwaunganishia wateja umeme katika maeneo husika, ambapo alisema gharama yake ni shilingi 27,000 tu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mfuru, Kata ya Kitete, Wilaya ya Kilosa, wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya umeme kwa Mkoa wa Morogoro, Jumatatu, Julai 9, 2018.
Mwakilishi wa Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Kusambaza umeme wilayani Kilosa, kupitia Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza (REA IIIA), Wingod Siyao kutoka Kampuni ya State Grid Electrical & Technical Works Ltd; akitoa ahadi mbele ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kilemba chekundu), kukamilisha Mradi huo kwa wakati. Naibu Waziri alikuwa katika ziara ya kazi kijijini Mfuru, Kata ya Kitete, Wilaya ya Kilosa, Jumatatu, Julai 9, 2018.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mandela, Kata ya Magole, Wilaya ya Kilosa, wakitoa maoni yao kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), wakati wa hafla ya kuzindua rasmi uwashaji wa umeme kupitia Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza (REA IIIA), kwa Mkoa wa Morogoro. Tukio hilo lilifanyika Jumatatu, Julai 9, 2018. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA
Hivyo makala Bilioni 45 kupeleka umeme kwa Vijiji 150 Morogoro
yaani makala yote Bilioni 45 kupeleka umeme kwa Vijiji 150 Morogoro Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Bilioni 45 kupeleka umeme kwa Vijiji 150 Morogoro mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/bilioni-45-kupeleka-umeme-kwa-vijiji.html
0 Response to "Bilioni 45 kupeleka umeme kwa Vijiji 150 Morogoro"
Post a Comment