Loading...
title : SPRITE BBALL KINGS YAANZA KUTIMUA VUMBI JIJINI DAR
link : SPRITE BBALL KINGS YAANZA KUTIMUA VUMBI JIJINI DAR
SPRITE BBALL KINGS YAANZA KUTIMUA VUMBI JIJINI DAR
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 hatua ya mchujo imemalizika kwa timu 15 kuingia hatua inayofuata baada ya michezo 25 kupigwa ndani ya Viwanja vya JMK Youth Park Kidongo Chekundu Jijini Dar es Salaam.
Mechi hizo zilizoanza saa 2 asubuhi ilizikutanisha timu 50 zote zikiwania nafasi ili ziweze kuingia hatua inayofuata ya 16 bora kuungana na mabingwa watetezi wa Mchenga BBall Stars.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF) Manase Zablon amesema timu hizo zilizofanikiwa kutinga hatua ya 16 bora wameweza kutumia vigezo vya utofauti wa alama za kushinda na kufungwa.
Manase amesema," mechi zilichezwa 25 na washindi 25 walipatikana katika mchezo vigezo vilivyotumika ili kuwapata wakaoenda hatua ya 16 bora tuliangalia utofauti wa vikapu vya kushinda na kufungwa."
Mchezaji wa timu ya St Joseph Jermaine Ishengoma akiifungua timu yake dhidi ya Madena Ballers. Ambapo St joseph aliibuka mshindi katika hatua ya mchujo uliofanyika jumamosi jijini Dar es salaam katika viwanja vya JMK Youth Park kidongo chekundu.
Mchezaji wa Oysterbay Godfrey Swai akijaribu kumtoka mchezaji wa Ilala East Zone Ally Salum Bakari wakati wa mashindano ya mpira wa kikapu ya sprite bball kings hatua ya mchujo uliofanyika jumamosi jijiji dar es salaam katika viwanja vya JMK Youth Park kidongo chekundu, Ambapo Timu ya Oysterbay iliibuka ushindi wa vikapu 48 kwa 19.
Mchezaji wa timu ya Montifort akijaribu kumshambulia mpinzani wake wa timu ya Goldent Talent wakati wa mashindano ya mpira wa kikapu ambapo tmt iliondoka na ushindi.Ambapo Timu ya Montifort iliibuka ushindi wa vikapu 24 dhidi ya 22 ya Goldent Talents.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala SPRITE BBALL KINGS YAANZA KUTIMUA VUMBI JIJINI DAR
yaani makala yote SPRITE BBALL KINGS YAANZA KUTIMUA VUMBI JIJINI DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SPRITE BBALL KINGS YAANZA KUTIMUA VUMBI JIJINI DAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/sprite-bball-kings-yaanza-kutimua-vumbi.html
0 Response to "SPRITE BBALL KINGS YAANZA KUTIMUA VUMBI JIJINI DAR"
Post a Comment