Loading...

TDB KUIKOPESHA TANZANIA SHILINGI BILIONI 900 KUJENGA RELI YA KATI YA KISASA NA MRADI WA UMEME KILWA

Loading...
TDB KUIKOPESHA TANZANIA SHILINGI BILIONI 900 KUJENGA RELI YA KATI YA KISASA NA MRADI WA UMEME KILWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TDB KUIKOPESHA TANZANIA SHILINGI BILIONI 900 KUJENGA RELI YA KATI YA KISASA NA MRADI WA UMEME KILWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TDB KUIKOPESHA TANZANIA SHILINGI BILIONI 900 KUJENGA RELI YA KATI YA KISASA NA MRADI WA UMEME KILWA
link : TDB KUIKOPESHA TANZANIA SHILINGI BILIONI 900 KUJENGA RELI YA KATI YA KISASA NA MRADI WA UMEME KILWA

soma pia


TDB KUIKOPESHA TANZANIA SHILINGI BILIONI 900 KUJENGA RELI YA KATI YA KISASA NA MRADI WA UMEME KILWA

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (Trade and Development Bank-TDB), itaikopesha Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya dola za Marekani milioni 400, sawa na takriban shilingi bilioni 900, kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) na Mradi wa kuzalisha umeme wa gesi wa Kilwa.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Rais wa Benki hiyo yenye Makao yake Makuu Jijini Nairobi Nchini Kenya, Bw. Admassu Tadesse, alipokutana na kufanya mazungunzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.

Bw. Tadesse amesema kuwa Benki yake imetenga kiasi cha dola za Marekani milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati ya kisasa pamoja na kiasi kingine kama hicho kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa gesi wa Kilwa mkoani Lindi.

"Tanzania ni mdau mkubwa wa Benki hii ikiwa inashika nafasi ya 7 kati ya nchi na taasisi 37 zinazomiliki hisa zake ambapo inamiliki hisa asilimia 6.4" alisema Bw. Tadesse.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (katikati) akijadiliana na ugeni wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika - TDB (hawamo pichani) kuhusu uboreshaji wa sekta ya nishati ya umeme ili kujenga uchumi wa viwanda.  Kulia ni Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Sauda Msemo.
 Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika –TDB, Bw. Admassu Tadesse (katikati) akitoa ufafanuzi wa mkopo wenye masharti nafuu utakaosaidia ujenzi wa Reli ya Kati ya Kiwango cha Kimataifa(SGR) na nishati ya umeme pamoja na miradi mingine midogomidogo. Kulia ni Mkuu wa Wakala wa Uendeshaji wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika –TDB Bi. Neema Siwingwa na kushoto ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Kisheria wa Benki hiyo Bw. David Bamlango.
 Ujumbe wa Serikali ya Tanzania (kulia) ukijadiliani na ujumbe wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika –TDB (kushoto) namna ya kufadhili ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa -(SGR) na Mradi wa kuzalisha Umeme kwa njia ya Gesi wa Kilwa.
  Ujumbe wa Serikali ya Tanzania (kulia) ukijadiliani na ujumbe wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika –TDB kwenye picha ya pamoja mara baada ya majadiliano ya namna Benki hiyo itakavyoikopesha Serikali kiasi cha dola milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa pamoja na Ujenzi wa mradi wa Umeme wa Gesi wa Kilwa utakaozalisha megawati 318 za umeme.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala TDB KUIKOPESHA TANZANIA SHILINGI BILIONI 900 KUJENGA RELI YA KATI YA KISASA NA MRADI WA UMEME KILWA

yaani makala yote TDB KUIKOPESHA TANZANIA SHILINGI BILIONI 900 KUJENGA RELI YA KATI YA KISASA NA MRADI WA UMEME KILWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TDB KUIKOPESHA TANZANIA SHILINGI BILIONI 900 KUJENGA RELI YA KATI YA KISASA NA MRADI WA UMEME KILWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/tdb-kuikopesha-tanzania-shilingi_10.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TDB KUIKOPESHA TANZANIA SHILINGI BILIONI 900 KUJENGA RELI YA KATI YA KISASA NA MRADI WA UMEME KILWA"

Post a Comment

Loading...