Loading...

TRA YAJA NA MKAKATI MAALUM KUONGEZA MAPATO KUPITIA SEKTA YA UTALII

Loading...
TRA YAJA NA MKAKATI MAALUM KUONGEZA MAPATO KUPITIA SEKTA YA UTALII - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TRA YAJA NA MKAKATI MAALUM KUONGEZA MAPATO KUPITIA SEKTA YA UTALII, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TRA YAJA NA MKAKATI MAALUM KUONGEZA MAPATO KUPITIA SEKTA YA UTALII
link : TRA YAJA NA MKAKATI MAALUM KUONGEZA MAPATO KUPITIA SEKTA YA UTALII

soma pia


TRA YAJA NA MKAKATI MAALUM KUONGEZA MAPATO KUPITIA SEKTA YA UTALII

Na Rachel Mkundai, Arusha

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha kwamba pato la Serikali na kodi stahiki inapatikana kupitia sekta ya utalii nchini.

Akizungumza Jijini Arusha, Kamishna wa Kodi za Ndani, Bwana ELIJAH MWANDUMBYAamesema kwamba, sekta ya utalii ni moja ya sekta inayoiingizia Serikali fedha nyingi za kigeni na hivyo inahitaji mkakati madhubuti ili kuongeza pato kwa Serikali

“Sekta ya utalii inaingizia serikali fedha nyingi za kigeni, TRA tumekuja na mkakati maalum ili kuhakikisha kuwa sekta hii inachangia pato la taifa kupitia kodi stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi”, amesema Kamishna wa kodi za ndani.

Mwandumbya ameongeza kuwa kwa muda mrefu sekta ya utalii imekuwa ikifanya vizuri lakini bado inahitaji mkakati wa kuhakikisha kwamba kila pato linaloingia kupitia sekta hii linaongeza tija kwenye mapato ya nchi kupitia kodi mbalimbali kama zilivyoainishwa na sheria za kodi.

Aidha, Kamishna Mwandumbya amefafanua kuwa moja ya mikakati hiyo ni kushirikiana na taasisi zingine za serikali zilizopo kwenye sekta ya utalii zikiwemo Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Chama cha wafanyabiashara wa Utalii (TATO) pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii na wadau wengine wanaojihusisha na utalii.
Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha, Bw. Faustine Mdesa (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara ya kikazi ya Kamishna wa Kodi za Ndani Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kulia) akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo (kushoto) akimwelezea jambo Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya pamoja na watendaji wengine wa TRA aliofuatana nao kuhusu namna sekta ya utalii nchini inavyochangia pato kubwa kwa Serikali wakati wa ziara ya kikazi ya Kamishna huyo Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini. (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA).



Hivyo makala TRA YAJA NA MKAKATI MAALUM KUONGEZA MAPATO KUPITIA SEKTA YA UTALII

yaani makala yote TRA YAJA NA MKAKATI MAALUM KUONGEZA MAPATO KUPITIA SEKTA YA UTALII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TRA YAJA NA MKAKATI MAALUM KUONGEZA MAPATO KUPITIA SEKTA YA UTALII mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/tra-yaja-na-mkakati-maalum-kuongeza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TRA YAJA NA MKAKATI MAALUM KUONGEZA MAPATO KUPITIA SEKTA YA UTALII"

Post a Comment

Loading...