Loading...
title : UTAFITI WABAINI KATIKA KILA HEKTA MOJA YA SHAMBA LA MPUNGA PANYA HUPOTEZA GUNIA TISA
link : UTAFITI WABAINI KATIKA KILA HEKTA MOJA YA SHAMBA LA MPUNGA PANYA HUPOTEZA GUNIA TISA
UTAFITI WABAINI KATIKA KILA HEKTA MOJA YA SHAMBA LA MPUNGA PANYA HUPOTEZA GUNIA TISA
UTAFITI uliofanywa na Chuo Kiku cha Sokoine (SUA) umeonesha kuwa katika kila hekta moja ya shamba la mpunga la umwagiliaji hupoteza gunia tisa za mpunga kutokana na kushambuliwa na panya.
Kwa mujibu wa SUA utafiti huo ulianza kufanyika mwaka 2015 baada ya chuo hicho kupata malalamiko mengi kutoka kwa wakulima wa zao la mpunga ambao walidai kuwa panya ndio adui yao mkubwa.
Akizungumzia utafiti huo jijini Dar es Salaam Profesa Loth Mulungu ambaye ni Mtafiti Mdhibiti wa viumbe hai na uharibifu amesema kutokana na utafiti huo hivi sasa tayari wamegundua vizuizi na mitego ambayo ni sumu kubwa kwa panya wanaokula mipunga katika mashamba.
Akifafanua zaidi kwenye Maonyesho ya 13 Vyuo Vikuu ya Elimu ya Juu Tanzania (TCU) yanayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Profesa Mulungu wanatumia vizuizi na mitego kwa ajili ya kuwakamata panya wanaoshambulia mpunga ambao tayari ulishakomaa katika shamba.
"Kwa siku tunatega panya zaidi ya mia mbili ambao hao wangekuwa wameingia kwenye shamba la mpunga wangekuwa wameshambilia zaidi mpunga ambao uliokuwa unasubiriwa kuvunwa,"amesema Profesa Malungu.
Pia amesema lengo lao kubwa ni kuongeza ufanisi katika uthibiti wa panya kwenye mashamba ya umwagiliaji na kwamba wadudu wengi waharibifu wakiwemo panya wanapenda kuvamia katika mashamba ya umwagiliaji kwa sababu mwaka mzima mashamba hayo yana mazao tofauti na yale mashamba yanayotegemea mvua za masika.
Hata hivyo amesema katika nchi ya Asia tayari wamefanikiwa kwa kutumia njia ya kuweka vizuizi na mitego katika mashamba ya panya."SUA tunataka kuipeleka teknolojia hiyo mpya katika mikoa inayolima mpunga kama vile Morogoro ,Iringa,Mvomero na Kilombero.
Hivyo makala UTAFITI WABAINI KATIKA KILA HEKTA MOJA YA SHAMBA LA MPUNGA PANYA HUPOTEZA GUNIA TISA
yaani makala yote UTAFITI WABAINI KATIKA KILA HEKTA MOJA YA SHAMBA LA MPUNGA PANYA HUPOTEZA GUNIA TISA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UTAFITI WABAINI KATIKA KILA HEKTA MOJA YA SHAMBA LA MPUNGA PANYA HUPOTEZA GUNIA TISA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/utafiti-wabaini-katika-kila-hekta-moja.html
0 Response to "UTAFITI WABAINI KATIKA KILA HEKTA MOJA YA SHAMBA LA MPUNGA PANYA HUPOTEZA GUNIA TISA"
Post a Comment