Loading...
title : WAKUU WA IDARA ZA KILIMO NA USHIRIKA WAAGIZWA KUUNDA USHIRIKA WA ZAO LA DENGU KATIKA HALMASHAURI YA ITIGI
link : WAKUU WA IDARA ZA KILIMO NA USHIRIKA WAAGIZWA KUUNDA USHIRIKA WA ZAO LA DENGU KATIKA HALMASHAURI YA ITIGI
WAKUU WA IDARA ZA KILIMO NA USHIRIKA WAAGIZWA KUUNDA USHIRIKA WA ZAO LA DENGU KATIKA HALMASHAURI YA ITIGI
Na Jumbe Ismailly- ITIGI
MWENEYEKITI wa Halmashauri ya Itigi,Wilayani Manyoni,Mkoani Singida,Ally Minja amewaagiza wakuu wa idara za Kilimo na Ushirika kuanzisha ushirika wa wakulima wa zao la dengu katika Halmashauri hiyo,ili kuwapunguzia wakulima wa zao hilo unyanyasaji wanaoupata wakati wanapotaka kuuza dengu kwa wafanyabiashara wa zao hilo.
Mwenyekiti huyo alitoa agizo hilo kwenye mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Kijiji cha Songambele,katika Mji mdogo wa Itigi,wilayani Manyoni.
Aidha Minja alisisitiza kwamba wakati umefika kwa Halmashauri hiyo kuwanasua wakulima wa dengu katika manyanyaso wanayopata kutoka kwa wanunuzi wa zao hilo waliojenga utamaduni wa kuwadhulumu haki zao kwa kutaka kuuziwa zao hilo likiwa bado lipo shambani.
“Tumechoka wakulima wa dengu kuendelea kunyanyaswa na kudhulumiwa,dengu kuendelea kununuliwa zikiwa bado shambani haitapendeza sana tunataka tuanzishe ushirika wa dengu”alisisitiza Mwenyekiti huyo.kusoma ZIDI BOFYA HAPA
Ni baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Itigi wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Kijiji cha Songambele,mjini Itigi wakiomba dua ya kuliombea baraza hilo kufanya maamuzi yenye hekma na busara.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi,Ally Minja(wa pili kutoka kulia) akiwaongoza madiwani wa Halmashauri hiyo katika dua ya kuliombea baraza hilo kufanya maamuzi yenye hekma na busara sambamba na kudumisha amani iliyopo nchini.
Makarani wa mikutano ya madiwani wakiwa katika ukumbi wa mikutano wakinukuu maazimio yanayopitishwa na wajumbe wa mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Kijiji cha Songambele.mjini Itigi.
Magunia ya zao la dengu yakiwa yamehifadhiwa kwenye ghala moja la mfanyabiashara wa mjini Itigi,yakisubiri kusafirishwa kwenda kwenye soka la zao hilo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).
Hivyo makala WAKUU WA IDARA ZA KILIMO NA USHIRIKA WAAGIZWA KUUNDA USHIRIKA WA ZAO LA DENGU KATIKA HALMASHAURI YA ITIGI
yaani makala yote WAKUU WA IDARA ZA KILIMO NA USHIRIKA WAAGIZWA KUUNDA USHIRIKA WA ZAO LA DENGU KATIKA HALMASHAURI YA ITIGI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKUU WA IDARA ZA KILIMO NA USHIRIKA WAAGIZWA KUUNDA USHIRIKA WA ZAO LA DENGU KATIKA HALMASHAURI YA ITIGI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/wakuu-wa-idara-za-kilimo-na-ushirika.html
0 Response to "WAKUU WA IDARA ZA KILIMO NA USHIRIKA WAAGIZWA KUUNDA USHIRIKA WA ZAO LA DENGU KATIKA HALMASHAURI YA ITIGI"
Post a Comment