Loading...
title : DAWASCO YAKAMATA WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI
link : DAWASCO YAKAMATA WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI
DAWASCO YAKAMATA WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) imekamata mashine za maji (pump) zilizokuwa zimeunganishwa kwenye mabomba ya shirika hilo na kuwauzia wananchi kinyume cha sheria. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa operesheni maalumu ya kufichua wezi wa maji Meneja wa DAWASCO wa Magomeni Mhandisi Damson Mponjoli amesema kuwa shirika halitaacha watu wanaohujumu shirika na kuathiri wananchi wengine wasipate maji.
Amesema kuwa licha waliojiunganishia maji kenyemela kukimbia lakini kidhibiti chao hakiwezi kukimbia hivyo hatua za kisheria zitafuata kwanza ni kujisarimisha kwenye mamlaka. Mhandisi Mponjoli amewaomba wajumbe wa serikali za mtaa kupeleka orodha ya watu 50 ili kuwawekea vizimba vya maji ili kuondoa adha ya upatikanaji wa maji katika maoeneo yao.
Amesema kuwa miundombinu yote iliyokuwa imeunganishwa lazima ifumuliwe kutokana na watu hao kuunganisha mabomba hayo na kupitisha katika katika vyoo na mitaro ya maji machafu. Mponjoli amesema kuwa yao walijiungia maji kiholela suala ambalo linahatarisha usalama wa afya za wananchi pamoja na shirika kukosa mapato ya kuendeshea huduma ya maji katika maeneo yao.
Katika operesheni hiyo wamekamata Mashine za Kuvuta Maji kutoka katika Mabomba makubwa ya dawasco, matanki Nane(8) ya Lita 10000,5000 na lita 2000. Operesheni imefanyika katika maeneo ya Magomeni Manzese, Manzese Midizini, Manzese Kilimahewa ampapo operesheni hiyo inaendelea maeneo mengine.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Mashine za kuvuta maji zilizokuwa zikitumika kuiba maji na kuyaweka kwenye matanki kwa ajili ya kuyauza.
Moja ya eneo zilipokuwa zimefungwa mashine.
Wananchi wakichota maji katika tanki la maji lililokuwa likijazwa na kuuziwa wananchi kwa shilingi 100/- kwa ndoo.
Hivyo makala DAWASCO YAKAMATA WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI
yaani makala yote DAWASCO YAKAMATA WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DAWASCO YAKAMATA WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/dawasco-yakamata-wahujumu-miundombinu.html
0 Response to "DAWASCO YAKAMATA WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI"
Post a Comment