Loading...
title : WANAFUNZI 200 SHULE MBALIMBALI ZA SEKONDARI KUONESHA KAZI ZAO ZA TEKNOLOJIA YA UGUNDUZI NA SAYANSI
link : WANAFUNZI 200 SHULE MBALIMBALI ZA SEKONDARI KUONESHA KAZI ZAO ZA TEKNOLOJIA YA UGUNDUZI NA SAYANSI
WANAFUNZI 200 SHULE MBALIMBALI ZA SEKONDARI KUONESHA KAZI ZAO ZA TEKNOLOJIA YA UGUNDUZI NA SAYANSI
JUMLA ya Wanafunzi 200 kutoka shule mbalimbali za sekondari nchini wanatarajiwa kuonesha kazi zao za teknolojia ya ugunduzi na sayansi kukabiliana na changamoto za maendeleo nchini.
Kazi hizo ziko katika nyanja za sayansi kama kemia,fizikia ,hesabu, baiolojia, mazingira, sayansi ya jamii na teknolojia.Maonesho ya kazi hizo za wanafunzi yameandaluwa na Taasisi inasaidia wanasayansi Chipukizi ya YST ikiwahusisha pia walimu 100 wakiambatana na wanafunzi hao ili kuonesha kazi hizo walizoziandaa kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Akizungumzia maonesho hayo yatakayofanyika Agosti 1 na 2 jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi Mwenza was YST ,Dr Gosbert Kamugisha alisema katika mashindano ya kazi hizo, wataonesha kazi za kigunduzi na wale watakaoshinda watapata udhamini wa kusoma masomo ya sayansi katika vyuo vya elimu ya juu.
Alisema lengo la maonesho hayo yaliyoanza kuoneshwa nchini tangu mwaka 2012 ,yatasaidia kuinua ari ya wanafunzi kusoma masomo ya sayansi jambo litakalosaidia kupata wataalam wengi katika eneo sayansi na kufanya kazi katika viwanda.
" wanasayansi hao ambao ni chipukizi watakaonesha ugunduzi mzuri wataawadiwa pesa taslimu,medali na vifaa vya maabara," alisema na kuongeza kuwa wanne watapewa ufadhili kusomeshwa elimu ya chuo kikuu ambao huyolewa na shirika la Karimjee,Jivanjee Foundation ili kuendelea kjimarisha vipaji vyao vya ugunduzi wa kisayansi.
Amesema maonesho hayo kuhamasisha wanafunzi was sekondari kupenda sayansi na ugunduzi na kujenga utamafuni was kisayansinkwa vijana was kitanzania,in fursa nzuri kwa wanafunzi was sekkndari kuonesha njia madhubuti za kukabiliana na chanhamoto za kijamii na kiuchumi.
Mwanzilishi Mwenza wa YST,Dk Gosbert Kamugisha (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wanafunzi 200 kutoka shule za sekondari nchini wanaotarajiwa kuonesha kazi zao za teknolojia Agosti 1,2 mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar as Salaam.
Mwanzilishi Mwenza wa shirika la YST,Joseph Clowry (kulia) akizungumza na waandishi wa habari juu ya maonesho yatayofanyika Agosti 1,2 mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar as Salaam.Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii.
Hivyo makala WANAFUNZI 200 SHULE MBALIMBALI ZA SEKONDARI KUONESHA KAZI ZAO ZA TEKNOLOJIA YA UGUNDUZI NA SAYANSI
yaani makala yote WANAFUNZI 200 SHULE MBALIMBALI ZA SEKONDARI KUONESHA KAZI ZAO ZA TEKNOLOJIA YA UGUNDUZI NA SAYANSI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI 200 SHULE MBALIMBALI ZA SEKONDARI KUONESHA KAZI ZAO ZA TEKNOLOJIA YA UGUNDUZI NA SAYANSI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/wanafunzi-200-shule-mbalimbali-za.html
0 Response to "WANAFUNZI 200 SHULE MBALIMBALI ZA SEKONDARI KUONESHA KAZI ZAO ZA TEKNOLOJIA YA UGUNDUZI NA SAYANSI"
Post a Comment