Loading...
title : WAZAZI, WALEZI WATAKIWA KUFICHUA WATOTO WENYE ULEMAVU
link : WAZAZI, WALEZI WATAKIWA KUFICHUA WATOTO WENYE ULEMAVU
WAZAZI, WALEZI WATAKIWA KUFICHUA WATOTO WENYE ULEMAVU
Na Frankius Cleophace, Serengeti
KATA ya Manchira wilayani Serengeti mkoani Mara wameendelea kuwabaini watoto wenye ulemavu wa aina yeyote ili wapelekwe shule kwa lengo la kupata haki zao kama watoto wengine.
Hivyo wazazi na walezi wilayani humo wametakiwa kuendelea kufichua watoto wenye ulemabu ili nao wapate haki ya kupata elimu.
Hayo yamebainishwa na Ofisa Elimu Kata ya Machira Fidel Sylivanus wakati wa tamasha lililoandaliwa na Shirika la RIGHT TO PLAY kwa lengo ni kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na mila zenye madhara ukiwemo ukeketaji kwa mtoto wa kike.Sylivanus amesema katika kata nzima tayari wamezunguka na kubaini watoto wenye ulemavu wa aina yeyote na kuwataka wazazi na walezi kufichua watoto hao.
Pia amewahamiza wazazi na walezi suala la elimu kwa watoto wote bila ubaguzi wa jinsia ni muhimu huku watoto wakitaja changamoto kubwa kuwa ni wazazi kuwapatia kazi nyingi na kushindwa kufanya michezo na kujisomea.Leah Kimaro kutoka Shirika la RIGHT TO PLAY amesema takribani Siku Nne amabazo shirika hilo limefanya matamasha wamefikia wananchi takribani 5000Elfu na kuweza kuwapatia ujumbe uliokusudiwa kupitia michezo mbalimbali.
Amesema michezo hiyo iliambatana na maombi, Ngonjera, Maigizo, Mpira wa miguu kwa watoto wakike, kukimbiza kuku na kukimbia ndani ya magumia na kwamba lengo ni kukusanya jamii ili kupatiwa elimu hiyo.Aidha wananchi wamekuwa na maoni tofauti kuhusu matamasha hayo ambao yameandaliwa na Shirika la RIGHT TO PLAY kwa siku nne na kutoa elimu ilikusudiwa katika jamii wilayani Serengeti mkoani Mara.
Ambapo wameomba kuwa matamasha hayo yawe endelevu katika maeneo ya vijijini ili kuendelea kutoa elimu Katika wilaya hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Miseke na Wananchi wakata ya Manchira Wilayani Serengeti Mkoani Mara wakiwa katika Maandamano na Mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kupiga Vita Ukatili kwa watoto kwenye Tamasha la Michezo lililoandaliwa na Shirika la RIGHT TO PLAY lililopo Serengeti Mkoani Mara.
Afisa Elimu kata ya Manchira Fidelis Sylivanus akisalimiana na Timu ya Mpira wa Miguu Miseke Wakubwa FC na Miseke Wadogo FC.
Afisa Elimu kata ya Manchira Fidelis Sylivanus akisalimiana na Timu ya Mpira wa Miguu wa Wasichana baina ya Timu Miseke FC na Bwitenge FC katika Viwanja vya Shule ya Msingi Miseke.
Mgeni rasmi ambaye ni Afisa Elimu Kata ya Manchira Fidels Syilivanusi akikabidhi zawadi mbalimbali kwa Washiriki wa Michezo hiyo.
Hivyo makala WAZAZI, WALEZI WATAKIWA KUFICHUA WATOTO WENYE ULEMAVU
yaani makala yote WAZAZI, WALEZI WATAKIWA KUFICHUA WATOTO WENYE ULEMAVU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZAZI, WALEZI WATAKIWA KUFICHUA WATOTO WENYE ULEMAVU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/wazazi-walezi-watakiwa-kufichua-watoto.html
0 Response to "WAZAZI, WALEZI WATAKIWA KUFICHUA WATOTO WENYE ULEMAVU"
Post a Comment