Loading...
title : WAZIRI MBARAWA AWATAKA WATAALAM WA DAWASA, DAWASCO KUTOA MAJIBU YA UPOTEVU WA MAJI
link : WAZIRI MBARAWA AWATAKA WATAALAM WA DAWASA, DAWASCO KUTOA MAJIBU YA UPOTEVU WA MAJI
WAZIRI MBARAWA AWATAKA WATAALAM WA DAWASA, DAWASCO KUTOA MAJIBU YA UPOTEVU WA MAJI
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
SERIKALI imewaagiza wataalamu kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) na Shirika la Majisafi na Majitaka (DAWASCO) kutoa majibu kuhusu upotevu wa maji unaosababisha hasara kubwa kwa Serikali.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Process Makame Mbarawa ameagiza hayo leo wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu ya maji iliyopo chini ya Dawasa ya Ruvu Juu na Ruvu chini.
Profesa Mbarawa ameeleza licha ya juhudi zinazofanywa na Serikali ya kumaliza tatizo la maji, Dar es Salaam na Pwani, asilimia 44 ya maji kati ya lita milioni 504 zinazozalishwa kila siku katika vyanzo mbali mbali hupotea kabla ya kufika kwa mtumiaji wa mwisho.
Kwa mujibu wa Waziri Mbarawa, takribani bilioni nne hupotea kila mwezi kutokana na upotevu wa maji hayo, upotevu ambao ni mkubwa wakati wananchi wakiwa hawana maji.
"Serikali inapoteza fedha nyingi kutokana na upotevu wa maji njiani kabla ua kufika kwa mtumiaji wa mwisho, ni wakati umefika sasa kwa wataalumu wetu kumaliza tatizo na kutoa majibu yanayoeleweka, lazima Tuingie kwa undani tuangalie maji haya yanapotelea wapi" amesema Profesa Mbarawa
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, akikagua mtambo wa Ruvu Chini, wakati wa ziara yake ya kikazi, Ruvu, mkoani Pwani.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamalaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Dk. Suphian Masasi, kuhusu mtambo wa mpya wa Ruvu Juu wa kudhalisha maji, mkoani Pwani.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kukagua kituo cha kusukuma maji ghafi katika mtambo wa Ruvu Juu, Mkoa wa Pwani.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamalaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Dk. Suphian Masasi, kuhusu kituo cha kusukuma maji ghafi katika mtambo wa Ruvu Juu, Mkoa wa Pwani.
Mkazi wa Kiluvya wilayani Ubungo akitoa malalamiko yake kuhusu mfumo wa kulipia maji unaotumiwa na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), unavyowasumbua wananchi kupata huduma ya majisafi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI MBARAWA AWATAKA WATAALAM WA DAWASA, DAWASCO KUTOA MAJIBU YA UPOTEVU WA MAJI
yaani makala yote WAZIRI MBARAWA AWATAKA WATAALAM WA DAWASA, DAWASCO KUTOA MAJIBU YA UPOTEVU WA MAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MBARAWA AWATAKA WATAALAM WA DAWASA, DAWASCO KUTOA MAJIBU YA UPOTEVU WA MAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/waziri-mbarawa-awataka-wataalam-wa.html
0 Response to "WAZIRI MBARAWA AWATAKA WATAALAM WA DAWASA, DAWASCO KUTOA MAJIBU YA UPOTEVU WA MAJI"
Post a Comment