Loading...
title : WAZIRI WA FEDHA AHIMIZA MAADILI TRA, AZUNGUMZIA UTOZAJI KODI KWA HAKI
link : WAZIRI WA FEDHA AHIMIZA MAADILI TRA, AZUNGUMZIA UTOZAJI KODI KWA HAKI
WAZIRI WA FEDHA AHIMIZA MAADILI TRA, AZUNGUMZIA UTOZAJI KODI KWA HAKI
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dk. Philipo Mpango ametoa onyo hatakuwa tayari kuona fedha ambazo zimepitishwa katika bajeti ya fedha ya mwaka 2018/2019 zikitumika kinyume na malengo yaliyokusudiwa na atakaebainika atachukuliwa hatua kali.
Mpango ametoa kauli hiyo jana alipotembelea banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ambapo alikutana na mkuu wa kitengo cha maadili na kutoa maagizo mbalimbali yakiwamo linalowataka watumishi wa kitengo hicho kufanya kazi kwa maadili.
Amefafanua kitengo hicho ni kitengo baba katika suala la maadili hivyo haitakiwi kuonekana mtumishi wake au wa idara nyingine akikiuka maadili ya kazi. Amewataka wasimamizi wa kitengo hicho wasicheze na nyoka na kwamba mtu anayekiuka maadili ya kazi hana tofauti na nyoka.
"Mnatakiwa kuwa wakali ili fedha za umma zisipotee. Bajeti ya serikali imepita na leo(jana)imetimiza siku tisa tangu mwaka mpya wa fedha uanze. Hivyo kuweni makini."Katika kitengo cha maadili watu nane wamefukuzwa kati ya watumishi 23.Na kwangu nitakuwa tayari kufukuza hata wote iwapo nitabaini maadili hayazingatiwi. Hivyo hakikiesheni mnasimama katika maadili ya kazi,"amesema.
Wakati huo huo amesema asilimia 60 ya Watanzania ni vijana hivyo wanatakiwa kuelimishwa mapema ili wawe na utamaduni wa kulipa kodi.
Pia amewatakaTRA kuhakikisha wanawapenda walipa kodi na kuwatoza kwa haki kulingana na shughuli anayoifanya.Amesisitiza kodi za wananchi zikusanywe vizuri kama ilivyopangwa ambapo akiwa hapo amewaleza TRA kuwa tarakimu za fedha zilizopo zinafurahisha lakini inatakiwa zifike ili zisaidie jamii.
Mpango amefafanua ni vema watumishi wa Idara hiyo kutambua kuwa kitengo hicho si sehemu ya kufanya mambo ya hovyo hovyo. "Najua ujumbe umetumwa na umefika,kuweni makini na fanyeni kazi kwa ajili ya taifa letu, "amesisitiza Mpango.
Hivyo makala WAZIRI WA FEDHA AHIMIZA MAADILI TRA, AZUNGUMZIA UTOZAJI KODI KWA HAKI
yaani makala yote WAZIRI WA FEDHA AHIMIZA MAADILI TRA, AZUNGUMZIA UTOZAJI KODI KWA HAKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI WA FEDHA AHIMIZA MAADILI TRA, AZUNGUMZIA UTOZAJI KODI KWA HAKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/waziri-wa-fedha-ahimiza-maadili-tra.html
0 Response to "WAZIRI WA FEDHA AHIMIZA MAADILI TRA, AZUNGUMZIA UTOZAJI KODI KWA HAKI"
Post a Comment