Loading...
title : ZFDA YATEKETEZA TANI 95 ZA CHAKULA NA TANI MOJA YA DAWA ZA BINADAMU ZILIZOMALIZA MUDA WA MATUMIZI
link : ZFDA YATEKETEZA TANI 95 ZA CHAKULA NA TANI MOJA YA DAWA ZA BINADAMU ZILIZOMALIZA MUDA WA MATUMIZI
ZFDA YATEKETEZA TANI 95 ZA CHAKULA NA TANI MOJA YA DAWA ZA BINADAMU ZILIZOMALIZA MUDA WA MATUMIZI
Na Ramadhani Ali, Maelezo Zanzibar
Mamlaka ya Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) imejidhatiti kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingizwa nchini zinawafikia wananchi zikiwa salama kwa matumizi kwa lengo la kulinda afya zao.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Usalama wa chakula wa ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar alieleza hayo katika jaa la Kibele wakati wa kazi ya kuangamiza tani 95 za bidhaa za mchele, sembe na Unga wa ngano pamoja na tani moja ya dawa za binadamu.
Alisema bidhaa za chakula zilizoangamizwa za mfanyabiashara Mohamed Mattar ziliharibika baada ya kuhifadhiwa kwa muda mrefu katika maghala yasiyorasmi na yaliyokosa sifa za kutumika kwa kazi hiyo.
Dkt. Khamis alieleza kuwa kutokana na maghala hayo kukosa viwango vinavyokubalika na kutosajiliwa na ZFDA, mfanyabiashara Mattar alikuwa akiweka bidhaa zake kwa siri wakati wa usiku.
Akitaja viwango vya bidhaa zilizoangamizwa, Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti na uhifadhi wa chakula wa ZFDA alisema mchele ulikua tani 52, unga wa ngano tani 37 na sembe ilikuwa tani sita.
Fundi wa mageti akikata geti la Ghala lililokua likihifadhiwa bidhaa za Mchele, Unga wa ngano na sembe uliomaliza muda na haufai kwa matimizi ya binadamu katika mtaa wa Migombani Mjini Zanzibar.
Sshemu ya bidhaa ya Mchele na Unga wa Ngano na Sembe zikiteremshwa katika magari kwa ajili ya Kuangamizwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.
Dawa za binadamu za aina mbali mbali za kuondosha maumivu na Virutubisho zilizo angamizwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
Gari la Kijiko likiangamiza Dawa za kuondosha maumivu na Virutubisho zilizoangamizwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkurungezi Idara ya Udhibiti na Usalama wa Vyakula wa ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar akizungamza na Waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuangamizaji Bidhaa zisizofa kwa Matumizi ya Binadamu lililofanyika katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Hivyo makala ZFDA YATEKETEZA TANI 95 ZA CHAKULA NA TANI MOJA YA DAWA ZA BINADAMU ZILIZOMALIZA MUDA WA MATUMIZI
yaani makala yote ZFDA YATEKETEZA TANI 95 ZA CHAKULA NA TANI MOJA YA DAWA ZA BINADAMU ZILIZOMALIZA MUDA WA MATUMIZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ZFDA YATEKETEZA TANI 95 ZA CHAKULA NA TANI MOJA YA DAWA ZA BINADAMU ZILIZOMALIZA MUDA WA MATUMIZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/zfda-yateketeza-tani-95-za-chakula-na.html
0 Response to "ZFDA YATEKETEZA TANI 95 ZA CHAKULA NA TANI MOJA YA DAWA ZA BINADAMU ZILIZOMALIZA MUDA WA MATUMIZI"
Post a Comment