Loading...

KALIUA YATOA PIKIPIKI 12 KWA MAOFISA UGANI ILI WAENDE KWA WAKULIMA

Loading...
KALIUA YATOA PIKIPIKI 12 KWA MAOFISA UGANI ILI WAENDE KWA WAKULIMA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KALIUA YATOA PIKIPIKI 12 KWA MAOFISA UGANI ILI WAENDE KWA WAKULIMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KALIUA YATOA PIKIPIKI 12 KWA MAOFISA UGANI ILI WAENDE KWA WAKULIMA
link : KALIUA YATOA PIKIPIKI 12 KWA MAOFISA UGANI ILI WAENDE KWA WAKULIMA

soma pia


KALIUA YATOA PIKIPIKI 12 KWA MAOFISA UGANI ILI WAENDE KWA WAKULIMA

Na Tiganya Vincent, Tabora
JUMLA ya watumishi 12 wa Kada mbalimbali wa Halmashauri ya  Wilaya ya Kaliua wakabidhiwa pikipiki zenye thamani ya milioni 29  kwa ajili ya kurahisisha utoaji huduma mbalimbali kwa wakulima na wananchi wanaoishi vijijini.

Akiongea kabla ya kukabidhi pikipiki hizo jana  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dkt. John Pima alisema kuwa lengo la utoaji pikipiki hizo ni kutaka Maofisa Ugani na Watendaji wa Kata waweze kuwafikia wakulima na wananchi mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia.

Alisema utoaji wa pikipiki hizo ni utekelezaji wa agizo la viongozi wa Kitaifa la kuwataka Maofisa Ugani kuondoka Ofisini na kwenda kwa wananchi kwa ajili ya kuwaelimisha juu kulima kilimo kilicho bora ambacho kitawawezesha kuzalisha kwa tija kwa ajili ya kuongeza kipato chao na kuwapata ziada kwa ajili ya kuuza.

Dkt. Pima alisema katika mwaka wa fedha walishatoa pikipiki 8 kwa ajili ya Maofisa Ugani Kata na Watenadaji wa Kata na wataendelea kununua pikipiki kwa kutumia mapato ya ndani hadi hapo watakapo hakikisha watumishi wa kada hiyo wanavyo vyombo vya usafiri kwa ajili ya kusaidia wananchi ikiwemo kulima kilimo bora na kusikiliza kero zao.

Alisema Halmashauri hiyo ili kuhakikisha inatekeleza agizo la viongozi imeshawasambaza Maofisa Ugani katika maeneo mbalimbali ya vijijini kwa ajili ya kuwasogeza karibu na wananchi ili watumie utaalamu wao kuwasaidia wakulima na sio kutoa maelekezo wakiwa ofisini.

Akikabidhi pikipiki Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alilipongeza Baraza la Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri hiyo kwa kutekeleza haraka agizo la viongozi wa kitaifa la kuwataka watendaji kwenda kusikiliza kero za wananchi.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akipanda pikipiki kabla ya kuzikabidhi jana kwa Watendaji wa Kata na Maofisa Ugani wa Kata mbalimbali wilayani Kaliua ili waende vijijini kutoa  huduma kwa karibu kwa wakulima na wananchi wengine.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kulia), Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele(katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama (kushoto) wakijaribu pikipiki kabla ya kukabidhi jana Watendaji wa Kata na Maofisa Ugani wa Kata mbalimbali wilayani Kaliua ili ziwasaidie kwenda kutoa huduma kwa karibu kwa wakulima na wananchi wengine. Picha na Tiganya Vincent.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala KALIUA YATOA PIKIPIKI 12 KWA MAOFISA UGANI ILI WAENDE KWA WAKULIMA

yaani makala yote KALIUA YATOA PIKIPIKI 12 KWA MAOFISA UGANI ILI WAENDE KWA WAKULIMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KALIUA YATOA PIKIPIKI 12 KWA MAOFISA UGANI ILI WAENDE KWA WAKULIMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/kaliua-yatoa-pikipiki-12-kwa-maofisa_16.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KALIUA YATOA PIKIPIKI 12 KWA MAOFISA UGANI ILI WAENDE KWA WAKULIMA"

Post a Comment

Loading...