Loading...
title : CHOMBO CHA USHINDANI WA BIASHARA KUANZA KAZI
link : CHOMBO CHA USHINDANI WA BIASHARA KUANZA KAZI
CHOMBO CHA USHINDANI WA BIASHARA KUANZA KAZI
Mamlaka ya Ushindani wa kibiashara kwa nchi za Afrika Mashariki yenye makao yake makuu Arusha, Tanzania inatarajiwa kuanza kusikiliza mashauri hasa yanayohusu kuunganisha kampuni.
Aidha, inaelezwa kuwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Tanzania ndiyo nchi yenye uzoefu wa muda mrefu zaidi katika kutekeleza sheria ya ushindani na utetezi wa mlaji.
Akizungumzia kipengele cha utetezi wa mlaji wakati wa semina hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani ya Tanzania (FCC), Dk John Kaduma alisema Kenya inashika nafasi ya pili huku Rwanda nayo ikiwa imepitisha sheria ya kuanzishwa kwa tume ya aina hiyo.
Uganda na Burundi zipo katika mchakato wa kuanzisha. Alisema sheria ya ushindani kwa nchi hizo ilitungwa mwaka 2006 na kanuni zake mwaka 2016 na tayari kuna mamlaka hiyo yenye ofisi zake mkoani Arusha.
Kaduma alisema katika kusikiliza mashauri kamati zitakazokaa zitakuwa chini ya mwenyekiti wa nchi husika, kwani wenyeviti wa kamati hizo zinahusisha viongozi wa taasisi za ushindani katika nchi husika.
Alisema nchini Tume ya Ushindani ilianza rasmi kutekeleza majukumu yake kama chombo chenye mamlaka kamili ya kusimamia sheria ya ushindani na sheria ya alama za bidhaa, inayotumika kudhibiti bidhaa bandia Mei 2007.
Naye Mkurugenzi wa Tafiti, Miungano ya Kampuni na Ushajihishaji Ushindani, Dk Allan Mlulla alitaja masuala ya msingi katika ushindani kuwa ni makubaliano yanayokiuka ushindani, matumizi mabaya ya nguvu ya soko, muungano wa kampuni.
Alisema ili kusimamia kwa ufanisi misingi ya ushindani katika uchumi wa soko, sheria ya ushindani imekataza makubaliano yanayokiuka ushindani, matumizi mabaya ya nguvu ya soko na miungano ya kampuni unaosababisha kuwepo au kuimarika kwa hodhi ya soko .
Alisema kwa mujibu wa sheria kampuni zinataka kuunganisha shughuli zao za kibiashara, ambazo thamani ya rasilimali zake kwa pamoja au mapato yao vinafikia 3,500,000,000 wanalazimika kuiarifu Tume kabla ya kuendelea na taratibu za kuunganisha shughuli zao
Naye Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia FCC, Zaytuni Kikula katika kudhibiti bidhaa bandia makontena 216 yaliyokuwa na bidhaa bandia yalikamatwa katika ukaguzi zinazofanyika na FCC bandarini katika mwaka wa fedha 2017/2018 yakiwa na bidhaa mbalimbali ikiwemo kofia ngumu za usalama za pikipiki.
Alisema katika kipindi hicho kumefanyika kaguzi 24 za kushtukiza katika kipindi hicho huku yakifanyika matukio manane ya kuteketeza bidhaa bandia nchini.
Alisema bidhaa zilizokamatwa ni pamoja na mabati, vipuri vya pikipiki, mashine na magari, kofia ngumu za usalama za pikipiki,viatu na miswaki. Kikula alisema mikakati mbalimbali inafanya kukabili bidhaa hizo, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha changamoto zilizopo zinafanyiwa kazi ikiwemi kukosekana kwa ofisi za kanda, wadau kushindw akuelewa au kupambanua tofauti ya majukumu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na FCC ne mengineyo.
Hivyo makala CHOMBO CHA USHINDANI WA BIASHARA KUANZA KAZI
yaani makala yote CHOMBO CHA USHINDANI WA BIASHARA KUANZA KAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CHOMBO CHA USHINDANI WA BIASHARA KUANZA KAZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/chombo-cha-ushindani-wa-biashara-kuanza.html
0 Response to "CHOMBO CHA USHINDANI WA BIASHARA KUANZA KAZI"
Post a Comment