Loading...
title : DC MJEMA ATANGAZA KIHAMA UHARIFU ILALA.
link : DC MJEMA ATANGAZA KIHAMA UHARIFU ILALA.
DC MJEMA ATANGAZA KIHAMA UHARIFU ILALA.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akiwa katika ziara yake ya wiki moja ambayo amameliza hivi karibu.
Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Kamati ya Ulinzi Wilaya ya Ilala inatarajia kukutana Agosti 2I mwaka huu kwa ajili ya kupanga Operesheni ya kwenda kuwakamata waharifu katika wilaya hiyo.
Akitoa taarifa ya tathmini ya ziara yake ya wiki moja leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema amesema kuwa baada ya kufanya ziara katika kata I3 ndani ya wilaya ya Ilala amebaini kuna idadi kubwa watu ambao wanafanya uharibifu katika jamii.
Mhe. Mjema amesema kuwa kuna watu wamekuwa na tabia mbalimbali ambazo sio rafiki katika jamii ikiwemo wizi, ubakaji jambo ambalo limekuwa likileta usumbufu mkubwa.
"Tayari majina ya waharifu tunayo kesho kamati ya ulinzi ikiwemo RPC wa Ilala tutakutana ili tupange operesheni ya kwenda kuwakamata waharifu wote waliopo ndani ya Wilaya ya Ilala" amesema Mhe. Mjema.
Mhe. Mjema ameeleza kuwa katika ziara hiyo kuna mambo mengi ambayo tumeyaona ikiwemo kero maji, utawala bora, Afya pamoja na miundombinu ya barabara.
"Nimepanga kusafisha uharifu katika Wilaya ya ilala, lakini maeneo ya ukonga imebainika kuna waharifu wengi sana" amesema Mhe. Mjema.
Mhe. Mjema ameeleza kuwa kila mtendaji anatakiwa kuendelea kutimiza majukumu yake ipasavyo ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana.
Hivyo makala DC MJEMA ATANGAZA KIHAMA UHARIFU ILALA.
yaani makala yote DC MJEMA ATANGAZA KIHAMA UHARIFU ILALA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC MJEMA ATANGAZA KIHAMA UHARIFU ILALA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/dc-mjema-atangaza-kihama-uharifu-ilala.html
0 Response to "DC MJEMA ATANGAZA KIHAMA UHARIFU ILALA."
Post a Comment