Loading...
title : FILAMU YA BAHASHA YAPATA MAPOKEZI MAKUBWA TOKA KWA WANANCHI
link : FILAMU YA BAHASHA YAPATA MAPOKEZI MAKUBWA TOKA KWA WANANCHI
FILAMU YA BAHASHA YAPATA MAPOKEZI MAKUBWA TOKA KWA WANANCHI
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Valentino Mlowola amesema njia nzuri ya kusambaza na kupeleka ujumbe kwa wananchi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa ni kutumia sanaa.
Mlolowa amesema hayo wakati wa uzinduzi wa filamu inayojulikana kwa jina la BAHASHA iliyoandaliwa na ubalozi wa Uswisi na Uholanzi kwa kushirikiana na Takukuru inayozungumzia madhara yanayojitokeza katika sehemu mbalimbali inayosababishwa na rushwa.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa filamu hiyo, Mlolowa amesema sanaa ni njia nzuri ya kuweza kufikisha ujumbe kwa urahisi kwakuwa wananchi wanapenda sana sanaa na filamu hii itawasaidia zaidi katika kuona madhara yanayokuja baada ya rushwa.
Amesema kuwa, filamu hii ina ujumbe mzuri sana na wanatarajia mwakani katika mbio za mwenge isambazwe ili nchi nzima ili wananchi waelewe madhara yatokanayo na rushwa na wananchi wameipokea kwa muitikio mkubwa sana.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Valentino Mlolowa akizungumza na wageni waalikwa waliofika katika uzinduzi wa filamu ya BAHASHA uliofanyika jana usiku Jijini Dar es Salaam.
Muandaaji wa Filamu hiyo Louise Kamin akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa filamu ya BAHASHA uliofanyika jana, filamu hiyo inayohusu Rushwa imewezwa kuandaliwa baina ya ubalozi wa Uswisi na Uholanzi pamoja Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU).
Waalikwa mbalimbali wakifuatilia kwa makini filamu ya BAHASHA iliyozunduliwa jana usiku na Ubalozi wa Uswisi kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi na Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Hivyo makala FILAMU YA BAHASHA YAPATA MAPOKEZI MAKUBWA TOKA KWA WANANCHI
yaani makala yote FILAMU YA BAHASHA YAPATA MAPOKEZI MAKUBWA TOKA KWA WANANCHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala FILAMU YA BAHASHA YAPATA MAPOKEZI MAKUBWA TOKA KWA WANANCHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/filamu-ya-bahasha-yapata-mapokezi.html
0 Response to "FILAMU YA BAHASHA YAPATA MAPOKEZI MAKUBWA TOKA KWA WANANCHI"
Post a Comment