Loading...

KASI YA UJENZI WA JENGO LA TRA PWANI HAIRIDHISHI -RC NDIKILO

Loading...
KASI YA UJENZI WA JENGO LA TRA PWANI HAIRIDHISHI -RC NDIKILO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KASI YA UJENZI WA JENGO LA TRA PWANI HAIRIDHISHI -RC NDIKILO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KASI YA UJENZI WA JENGO LA TRA PWANI HAIRIDHISHI -RC NDIKILO
link : KASI YA UJENZI WA JENGO LA TRA PWANI HAIRIDHISHI -RC NDIKILO

soma pia


KASI YA UJENZI WA JENGO LA TRA PWANI HAIRIDHISHI -RC NDIKILO

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI .

MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa jengo la mamlaka ya mapato Tanzania, (TRA) mkoani humo ,ujenzi ambao unasuasua kwa miaka miwili sasa na kubaki gofu.
Aidha amesema jengo hilo hadi lilipofikia halilingani na thamani ya sh.bilioni 1.653.267 .510 ambayo ni awamu ya kwanza iliyofikia asilimia 61 hadi sasa. 

Kufuatia hali hiyo ,Ndikilo amemuelekeza meneja wa mamlaka hiyo mkoa ,kumfikishia salamu kamishna wa mamlaka ya mapato makao makuu kufuatilia mradi wa ujenzi huo . 

Mkuu huyo wa mkoa alieleza masikitiko hayo ,wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa viwanja ya taasisi binafsi na serikali katika halmashauri ya Mji wa Kibaha,ikiwemo Uhamiaji,TRA na CRDB. Alisema ,lengo la kupewa viwanja hivyo ni kujenga maeneo hayo na sio kukumbatia viwanja bila sababu za msingi.

“Serikali ya mkoa na waziri mkuu Kassim Majaliwa ilishatoa agizo tangu mwaka juzi kuwa maeneo hayo yote yahakikishwe yanajengwa na kama haiwezekani wanyanganywe wahusika na kupewa wengine wenye uwezo” alisisitiza Ndikilo. Ndikilo alishangazwa na kupewa taarifa pia kuwa ujenzi huo bado unahitaji zaidi ya milioni 200 wakati hatua ya kwanza haiendani na maelekezo ya serikali na mkoa. “Gharama imesemwa itakuwa bilioni 2.693.402.120 ,ambapo mkandarasi Humphrey Construction Ltd, bado anahitaji fedha zaidi ambayo itafikia bilioni 2.8 jambo ambalo haliniingii akilini'” .

“Kwanza mmeshaezeka mabati Leo hii mnaniambia mtaendelea na hatua nyingine ya ujenzi kwa ghorofa tatu ambapo mtaondoa mabati ambayo yameshagharamiwa halafu muongeze majengo tena , haiwezekani nitaagiza vyombo vyangu vya ulinzi na usalama vichunguze zaidi, ” alifafanua Ndikilo .


Jengo la mamlaka ya mapato mkoani Pwani ambalo linasuasua katika ujenzi wake ambao ulitakiwa kukamilika tangu june 2016 .(picha na Mwamvua Mwinyi).
Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo alipotembelea jengo la idara ya uhamiaji mkoani Pwani ambalo limekamilika kwa gharama ya bilioni 1.6(picha na Mwamvua Mwinyi) .
Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo(kulia) alipotembelea ujenzi wa jengo la CRDB mkoani Pwani ambalo limekamilika kwa gharama ya milioni 900 , mbele kulia meneja CRDB Pwani Rosemary Nchimbi. (picha na Mwamvua Mwinyi



Hivyo makala KASI YA UJENZI WA JENGO LA TRA PWANI HAIRIDHISHI -RC NDIKILO

yaani makala yote KASI YA UJENZI WA JENGO LA TRA PWANI HAIRIDHISHI -RC NDIKILO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KASI YA UJENZI WA JENGO LA TRA PWANI HAIRIDHISHI -RC NDIKILO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/kasi-ya-ujenzi-wa-jengo-la-tra-pwani.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KASI YA UJENZI WA JENGO LA TRA PWANI HAIRIDHISHI -RC NDIKILO"

Post a Comment

Loading...