Loading...
title : Kesi ya Mgogoro ardhi wananchi wa Vicheji na AG yaahirishwa hadi Oktoba 11
link : Kesi ya Mgogoro ardhi wananchi wa Vicheji na AG yaahirishwa hadi Oktoba 11
Kesi ya Mgogoro ardhi wananchi wa Vicheji na AG yaahirishwa hadi Oktoba 11
Na Hussein Ndubikile, Mwambawahabari, Pwani
Baraza la Ardhi na Nyumba la Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani limeahirisha Kesi ya msingi ya mgogoro wa ardhi kati ya walalamikaji kutoka Kijiji cha Vicheji kiichopo wilayani dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG), Aderladus Kilangi kutokana na wakili upande wa walalamikaji kushindwa kufika sababu ya kuendelea kuuguza jeraha la mkono alilopata ajalini.
Mara mwisho Mwenyekiti wa Baraza hilo, Rehema Mwakibuja aliwaondoa wadaiwa wawili akiwemo Omari Issa na Bakari Saguti katika kesi hiyo kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG), Adelardus Kilangi ambaye ni mdaiwa dhidi ya walalamikaji zaidi ya 70 licha ya wadaiwa hao kudai hawawezi kutoa maelezo sababu kuwa Wakili wao hayupo.
Katika kesi hiyo Wakili wa mdaiwa, Daudi Mginge alimwambia mwenyekiti wakili upande walalamikaji amekuwa akishindwa kufika barazani hapo hali inayochelewesha usikilizaji wa kesi hivyo mwenyekiti alimtaka wakili,Maginge akathibitishe kama kweli wakili huyo amelazwa katika Hospitali ya Burele, mkoani Njombe.
Baada ya hapo wakili Daudi alimweleza Mwenyekiti kuwa walalamikaji wanatakiwa kulipa Sh 100,000 ya uahirishaji kesi na kusisitiza hakupata kielezo original cha uahirishaji kesi.
Wakili Daudi aliushauri upande wa walalamikaji kutafuta wakili mwingine au watafute mwakilishi atakayewakilisha kwenye usikilizaji wa kesi hiyo.
Kwa upande wake, mlalamikaji, Said Kais alisema bado wanaendelea na mazungumzo na wakili mwingine.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa baraza hilo aliuambia upande wa walalamikaji endapo utashindwa kushindwa na wakili wao atafuta kesi hiyo.
Mgogoro katika kesi namba 55 ya mwaka 2016 unawahusisha wadaiwa Said Kaisi 46, Bakari Saguti 60, Omary Issa 42, Juma Omary 40, Salima Bilali (53), Regia Issaya(55) ,Sada Abdallah(72) ambao kwa pamoja wanadaiwa kuingia kwenye shamba la Kilangi bila kibali.
Washitakiwa hao kwa pamoja inadaiwa kuwa Mei 9 2016 katika Kijiji cha Vicheji waliharibu Miti 13 ya Minazi na nyumba mbili vyenye thamani ya Sh. Mil 22.2 mali ya AG Kilangi.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa upande wa walalamikaji.
Hivyo makala Kesi ya Mgogoro ardhi wananchi wa Vicheji na AG yaahirishwa hadi Oktoba 11
yaani makala yote Kesi ya Mgogoro ardhi wananchi wa Vicheji na AG yaahirishwa hadi Oktoba 11 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kesi ya Mgogoro ardhi wananchi wa Vicheji na AG yaahirishwa hadi Oktoba 11 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/kesi-ya-mgogoro-ardhi-wananchi-wa.html
0 Response to "Kesi ya Mgogoro ardhi wananchi wa Vicheji na AG yaahirishwa hadi Oktoba 11"
Post a Comment