Loading...

SIKU YA 3 ; ZIARA YA MTAA KWA MTAA YA DC MJEMA YAWAKUNA WANANCHI WA

Loading...
SIKU YA 3 ; ZIARA YA MTAA KWA MTAA YA DC MJEMA YAWAKUNA WANANCHI WA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SIKU YA 3 ; ZIARA YA MTAA KWA MTAA YA DC MJEMA YAWAKUNA WANANCHI WA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SIKU YA 3 ; ZIARA YA MTAA KWA MTAA YA DC MJEMA YAWAKUNA WANANCHI WA
link : SIKU YA 3 ; ZIARA YA MTAA KWA MTAA YA DC MJEMA YAWAKUNA WANANCHI WA

soma pia


SIKU YA 3 ; ZIARA YA MTAA KWA MTAA YA DC MJEMA YAWAKUNA WANANCHI WA





Na Mwandishi wetu, Ilala
Mwambawahabari
Ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Mjema imewakuna wananchi wa Gongolamboto baada ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Gongolambo Bakari Shingo  kuvuliwa nafasi yake ya uenyekiti kwa mujibu wa sheria.


Hayo yamejijiri jana katika Ziara ya Mkuu wa Wilaya alipokuwa akizungumza na wakazi wa gongolamboto ambao wengi wao walitoa malalamiko dhidi ya Mwenyekiti huyo anayetokana na Chama Cha Wananchi CUF kushindwa kusimamia Masuala ya ulinzi na usalama na hivyo kupelekea vitendo vingi vya kihalifu katika mtaa huo.


Aidha, mwenyekiti alishutumiwa kushirikiana na wahalifu hao hivyo kushindwa kuchukua hatua.

Mmoja wa viongozi wa CUF katika mtaa huo alisema tayari mwenyekiti huyo alishafukuzwa rasmi uanachama kwani alikuwa akionywa juu ya vitendo vyake lakini hakubadilika.

Kwa upande wake Afisa Utumishi wa Manipsaa ya  Ilala ndugu William alieza kuwa “kutokana na taarifa hiyo ya kuvuliwa uanachama kwa mwenyekiti huyo basi automatically anakuwa siyo mwenyekiti tena”.

Mjadala huo uliibua shangwe na vifijo pale DC mjema alipohitimisha kwamba Gongolamboto sasa hatuna mwenyekiti na kuwataka chama husika kukamilisha mchakato wa kuwasilisha barua kwa Mkurugenzi kama taratibu zinavyotaka kumtaarifu uamuzi huo.

Sambamba na hilo Mjema alieleza kuwa suala la ulinzi na usalama ni ajenda ya kudumu katika mitaa yetu hivyo kila mwenyekiti anapaswa kuhakikisha kwamba anafanya vikao na kamati yake ya ulinzi na usalama mara kwa mara ili kupanga na kutekeleza mipango ya ulinzi katika mitaa yao. Pia, aliwataka wananchi hao kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano ya Rais Magufuli ambayo ina dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo kwa wananchi.



Aidha, DC Mjema amewataka mamlaka ya usimamizi wa barabara TARULA kusimamia ipasavyo barabara kuhakikisha zinapitika, wataalamu wa mazingira kusimamia ipasavyo suala la usafi huku akiwahimiza wanawake na vijana kuchangamkia fursa za tenda za uzoaji wa taka kwenye maeneo yao, sambamba na kuchangamkia fursa zinazopatikana kupitia mifuko 19 ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Mambo mengine ambayo Mjema ametoa maelekezo kushughulikiwa kwa haraka yanagusa sekta ya maji, mifugo, biashara.

Hii ni ziara maalamu ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwenye kata zote za Wilaya yake kuhamasisha shughuli za maendeleo, kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi ili kuzipatia ufumbuzi.
Katika ziara hii, mjema anaambatana na jopo la wataalamu wa ardhi, maji, barabara, maendeleo na Ustawi wa Jamii, Tanesco na idara zingine za serikali kutoa majibu ya maswali na kero za wananchi.

Leo ziara hiyo, inaendelea katika kata za Pugu na Pugu Station.


Hivyo makala SIKU YA 3 ; ZIARA YA MTAA KWA MTAA YA DC MJEMA YAWAKUNA WANANCHI WA

yaani makala yote SIKU YA 3 ; ZIARA YA MTAA KWA MTAA YA DC MJEMA YAWAKUNA WANANCHI WA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SIKU YA 3 ; ZIARA YA MTAA KWA MTAA YA DC MJEMA YAWAKUNA WANANCHI WA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/siku-ya-3-ziara-ya-mtaa-kwa-mtaa-ya-dc.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SIKU YA 3 ; ZIARA YA MTAA KWA MTAA YA DC MJEMA YAWAKUNA WANANCHI WA"

Post a Comment

Loading...