Loading...
title : KITILYA NA WENZAKE WAENDELEA KUSOTA RUMANDE
link : KITILYA NA WENZAKE WAENDELEA KUSOTA RUMANDE
KITILYA NA WENZAKE WAENDELEA KUSOTA RUMANDE
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
Aliyekuwa kamishna wa TRA, Harry Kitilya na waliokuwa maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Mori Sinare na Sioi Graham Solomon wanaokabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha.
wanaendelea kusota rumande kwa takribani miaka miwili sasa. Huku upelelezi wa kesi yao ukiwa bado haujakamilika. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa upelelezi bado haujakamilika ila upo katika hatua za kukamilika,
Baada ya kueleza hayo. Wakili wa utetezi Nsangizyo Nzilahulula alidai kuwa kumekuwepo na kauli za upande wa mashtaka kuwa bado kidogo wakamilishe upelelezi katika kesi hiyo ambazo ni zaidi ya mwaka sasa.
Na hakuna chochote kinachoendelea, hivyo aliiomba mahakama iwasaidie.
Baada ya kutolewa kwa Maelezo hayo , Wakili Kishenyi alieleza kuwa maombi ya kuomba msaada wa mahakama ni mapema sana kwa kuwa wanafafanya jitihada za kukamilisha upelelezi.
Hakimu Shaidi baada ya kusikiliza hoja za pande zote, amesema ameishafanya mazungumzo na upande wa mashtaka na kwamba kuna maagizo Fulani wanayafanyia kazi.
Kesi imeahirishwa hadi Agosti 31,2018.
Katika kesi hiyo, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha.
Washtakiwa hao, Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani 550 milioni kwa serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard Uingereza.
Wanadaiwa kuwa Machi 2013 jijini Dar es Salaam walijipatia Dola za Marekani 6 milioni, wakionyesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo na zililipwa kupitia Kampuni ya Egma T Ltd.
Washtakiwa hao wanadaiwa kutakatisha fedha kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka kiasi cha Dola za Marekani 6 milioni katika akaunti tofauti tofauti za benki.
Hivyo makala KITILYA NA WENZAKE WAENDELEA KUSOTA RUMANDE
yaani makala yote KITILYA NA WENZAKE WAENDELEA KUSOTA RUMANDE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KITILYA NA WENZAKE WAENDELEA KUSOTA RUMANDE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/kitilya-na-wenzake-waendelea-kusota.html
0 Response to "KITILYA NA WENZAKE WAENDELEA KUSOTA RUMANDE"
Post a Comment