Loading...
title : KOCHA SIMBA AIFIKIRIA MTIGWA SUGAR
link : KOCHA SIMBA AIFIKIRIA MTIGWA SUGAR
KOCHA SIMBA AIFIKIRIA MTIGWA SUGAR
Kocha Mkuu wa Simba Sport Club Patric Aussems.
Kocha Simba, Patrick Aussems ameutaja mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa kuwa utatoa taswira nzima ya walivyojipanga kwa ajili ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa jijini Mwanza Agosti 18, mwaka huu na baadaye ligi itaanza Agosti 22, mwaka huu. Akizungumza na gazeti hili Aussems alisema anajiandaa dhidi ya mchezo huo na mingine yote, lakini kikubwa ni namna gani wanajipanga kupata matokeo mazuri.
“Kuna michezo mitatu itanipa picha halisi namna tulivyojiandaa kwa ligi, tukicheza na Namungo ya Lindi tutaenda Mwanza kisha baadaye Arusha, ambako majibu yatakuwa yameshapatikana,”alisema.
Kocha huyo mwenye umbo kubwa kama wacheza mieleka alisema anatarajia kikosi chake kitakuwa moto baada ya kukamilisha maandalizi yote.
Wekundu hao wapo mkoani Lindi kwa mualiko maalum wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakitarajiwa kucheza mchezo wa kirafi ki dhidi ya timu ya Daraja la Kwanza ya Namungo katika uzinduzi wa uwanja.
Simba hivi karibuni walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana, mchezo wa kirafi ki wa kuadhimisha Simba Day uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Aussems alizungumzia namna alivyoridhishwa na kikosi chake tangu wakiwa kwenye mazoezi ya maandalizi ya msimu nchini Uturuki akivutiwa pia, na tabia njema waliyoimudu ndani na nje ya uwanja
Hivyo makala KOCHA SIMBA AIFIKIRIA MTIGWA SUGAR
yaani makala yote KOCHA SIMBA AIFIKIRIA MTIGWA SUGAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KOCHA SIMBA AIFIKIRIA MTIGWA SUGAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/kocha-simba-aifikiria-mtigwa-sugar.html
0 Response to "KOCHA SIMBA AIFIKIRIA MTIGWA SUGAR"
Post a Comment