Loading...
title : Kofi Annan, Katibu Mkuu wa Zamani wa Umoja wa Mataifa Aaga Dunia Akiwa na Miaka 80
link : Kofi Annan, Katibu Mkuu wa Zamani wa Umoja wa Mataifa Aaga Dunia Akiwa na Miaka 80
Kofi Annan, Katibu Mkuu wa Zamani wa Umoja wa Mataifa Aaga Dunia Akiwa na Miaka 80
Aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ameaga dunia akiwa na miaka 80.
Annan alikuwa ni mwafrika mweusi wa kwanza kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, akihudumu mihula miwili kuanzia mwaka 1997 hadi 2006.
Baadaye akahudumu kama mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria na kuchangia kupatikana kwa suluhu la amani la mzozo wa nchi hiyo.
Katika taarifa iliyotangaza kufariki kwake, wakfu wa Kofi Annan ulimtaja kama mtu aliyejitolea sana katika masuala ya kimataifa mbaye katika maisha yake yote alipigania kuwepo ulimwengu wenye amani.
Muhula wa Annan kama katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ulikumbwa na vita vya Iraq na janga la virusi vya HIV na Ugonjwa wa ukimwi.
Mambo makuu katika maisha ya Kofi Annan:
1938: Alizaliwa Kumasi ambao sasa ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Ghana
1962: Alianza kufanya kazi kwennye Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswzi
1965: Akamuoa Titi Alakija. Wana watoto wawili mvulana na msichana
1984: Akamuoa Nane Lagergren, baada ya talaka mwaka uliotangulia
1991: Dada yake ambaye ni pacha Efua afariki
1993: Akawa mkuu wa oparesheni za kulinda amani
1997: Ateuliwa katibu mkuu wa saba wa Umoja wa Mataifa
2001: Ashinda tuzo la amani
2006: Aondoka ofisini kama katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa baada ya kuhudumu miaka 10
Kofi Annan ni nani?
Kofi Atta Annan na dada yake Efua Atta, walizaliwa kwenye mji wa Kumasi katika nchi ambayo wakati huo ilikuwa inajulikana kama Gold Coast Aprili mwaka 1938. Majina ya pacha hao yaliamaanisha kuwa walizaliwa Ijumaa huku majina yao ya kati yakimaamisha kuwa waliukuwa ni pacha.
Alikulia kwenye familia ya kitajiri - mababu zake walikuwa ni viongozi wa kitamaduni na baba yake alikuwa ni gavana wa mkoa wakati nchi bado ilikuwa chini ya utawala wa ukoloni wa Uingereza
Siku mbilii tu kabla ya Kofi kihitimu miaka 19 nchi ikapata Uhuru wake na kuwa Ghana.
Hivyo makala Kofi Annan, Katibu Mkuu wa Zamani wa Umoja wa Mataifa Aaga Dunia Akiwa na Miaka 80
yaani makala yote Kofi Annan, Katibu Mkuu wa Zamani wa Umoja wa Mataifa Aaga Dunia Akiwa na Miaka 80 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kofi Annan, Katibu Mkuu wa Zamani wa Umoja wa Mataifa Aaga Dunia Akiwa na Miaka 80 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/kofi-annan-katibu-mkuu-wa-zamani-wa.html
0 Response to "Kofi Annan, Katibu Mkuu wa Zamani wa Umoja wa Mataifa Aaga Dunia Akiwa na Miaka 80"
Post a Comment