Loading...

MAHAKAMA KUU KANDA MBEYA YAPATA JAJI MFAWIDHI

Loading...
MAHAKAMA KUU KANDA MBEYA YAPATA JAJI MFAWIDHI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAHAKAMA KUU KANDA MBEYA YAPATA JAJI MFAWIDHI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAHAKAMA KUU KANDA MBEYA YAPATA JAJI MFAWIDHI
link : MAHAKAMA KUU KANDA MBEYA YAPATA JAJI MFAWIDHI

soma pia


MAHAKAMA KUU KANDA MBEYA YAPATA JAJI MFAWIDHI


Na Rajabu Singana, Mahakama Kuu Mbeya

Watumishi wa Mahakama Kanda ya Mbeya wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano bila kujali vyeo na kufanya kazi kama timu moja, kupendana na kufuata C tatu yaani ‘Coordination, Cooperation na Consultation’ ili kuwahudumia wananchi ipasavyo.

Hayo yalisemwa na Jaji Mfawidhi mpya wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba alipokuwa akiongea na Watumishi wa Kanda hiyo baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi Agosti, 15 2018, katika ofisi za Mahakama Kuu mkoani Mbeya.

Mhe. Jaji Makaramba alisisitiza viongozi wa ngazi ya juu ya Kanda hiyo yaani Jaji Mfawidhi, Naibu Msajili na Mtendaji wa Mahakama kufanya kazi kwa kufuata kile alichokiita ‘utatu mtakatifu’. 

Aidha, pamoja na mambo mengine, Mhe. Makaramba alisisitiza juu ya nidhamu na uadilifu wa watumishi wa Mahakama huku akikemea Watumishi kutojihusisha na vitendo vya rushwa ili kwa pamoja kuweza kufikia malengo ya Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015-2020) wa Mahakama. 

“Mtumishi akikamatwa kwa tuhuma za rushwa nitamsindikiza mwenyewe hadi TAKUKURU nikifika nawakabidhi wamalizane naye wenyewe” alisema Jaji Mfawidhi huyo.
Mhe Jaji Makaramba akisaini kitabu cha wageni.
Mhe. Dkt. Levira akisoma taarifa ya makabidhiano ya ofisi.
 
Watumishi wakimsikiliza Mhe. Makaramba (hayupo pichani)
Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kanda ya Mbeya, (wa tatu kushoto) ni Mhe. Jaji Paul Joel Ngwembe, (wa pili kulia) ni Mhe. Dkt. Mary Caroline Levira, wa kwanza kulia ni Naibu Msajili-Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. George Herbert, wa pili kushoto ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. William Mutaki na wa kwanza kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Bw. Moses Mwidete.



Hivyo makala MAHAKAMA KUU KANDA MBEYA YAPATA JAJI MFAWIDHI

yaani makala yote MAHAKAMA KUU KANDA MBEYA YAPATA JAJI MFAWIDHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA KUU KANDA MBEYA YAPATA JAJI MFAWIDHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/mahakama-kuu-kanda-mbeya-yapata-jaji.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAHAKAMA KUU KANDA MBEYA YAPATA JAJI MFAWIDHI"

Post a Comment

Loading...