Loading...

DK.BASHIRU KUTUA ZANZIBAR KWA MARA YA KWANZA.

Loading...
DK.BASHIRU KUTUA ZANZIBAR KWA MARA YA KWANZA. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DK.BASHIRU KUTUA ZANZIBAR KWA MARA YA KWANZA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DK.BASHIRU KUTUA ZANZIBAR KWA MARA YA KWANZA.
link : DK.BASHIRU KUTUA ZANZIBAR KWA MARA YA KWANZA.

soma pia


DK.BASHIRU KUTUA ZANZIBAR KWA MARA YA KWANZA.

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Bashiru Ally anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku nne visiwani humu Agosti 17 hadi 20 mwaka huu.

Dk.Bashiru anafanya ziara hiyo kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo Mei mwaka huu baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Abdulrahman Omar Kinana kustaafu.

Akitoa taarifa ya ziara hiyo ya Katibu Mkuu huyo, Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu Taifa(NEC),Idara ya Itikadi na Uenezi CCM, Zanzibar Catherine Peter Nao, alisema CCM Zanzibar tayari kimekamilisha maandalizi yote ya mapokezi ya kiongozi huyo.

Catherine alisema katika ziara yake hiyo pamoja na mambo mengine anatarajia kuzungumza na viongozi mbalimbali wa CCM na jumuiya zake na makundi ya kutoka taasisi za vijana visiwani humu.

Aliongeza kuwa ziara hiyo ya Dk.Bashiru itakuwa ni ya kikazi na kujitambulisha kwa wana-CCM ambapo wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Katibu Mkuu huyo ambapo atawahutubia wanachama pamoja na wananchi kwa ujumla katika uwanja wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui saa 9 alasiri.

“Tunawaomba wanachama wote tujitokeze kwa wingi kushiriki mapokezi hayo ya kiongozi wetu mpendwa ambaye ni mara ya kwanza kuja tukitambulisha na kuzungumzia sera na masuala mbalimbali ya kuimarisha CCM na Jumuiya zake, alisema Catherine.

Akizungumzia ratiba ya ziara hiyo Katibu huyo wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar,Catherine alisema siku ya siku ya kesho Agosti 17 mwaka huu katibu Mkuu huyo atakutana na kuzungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.

Katibu huyo aliongeza kuwa Dk.Bashiru anatarajia kukutana na na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.

KUSOMA ZAIDI BOFYUA HAYA>>>>>>


Hivyo makala DK.BASHIRU KUTUA ZANZIBAR KWA MARA YA KWANZA.

yaani makala yote DK.BASHIRU KUTUA ZANZIBAR KWA MARA YA KWANZA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DK.BASHIRU KUTUA ZANZIBAR KWA MARA YA KWANZA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/dkbashiru-kutua-zanzibar-kwa-mara-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DK.BASHIRU KUTUA ZANZIBAR KWA MARA YA KWANZA."

Post a Comment

Loading...