Loading...
title : MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA) YAKUTANA NA WADAU KUJADILI UDHIBITI WA GESI TIBA NCHINI
link : MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA) YAKUTANA NA WADAU KUJADILI UDHIBITI WA GESI TIBA NCHINI
MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA) YAKUTANA NA WADAU KUJADILI UDHIBITI WA GESI TIBA NCHINI
Picha ya pamoja baina ya viongozi wa TFDA na wadau wa gesi tiba kutoka Serikalini na sekta binafsi nchini. waliokaa kutoka kulia ni Meneja Majaribio na Usalama wa Dawa wa TFDA, Bi Kissa Mwamwitwa aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA (wa pili), Meneja wa Vifaa Tiba, Vitendanishi na Vipodozi wa TFDA, Bi Grace Shimwela (wa tatu), Mwenyekiti mteule wa kikao hicho, Eng. Daudi Mlwale (wa kwanza) na Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. 2. Msajili wa Dawa Mkuu wa TFDA, Bi. Rose Aaron akisisitiza jambo katika mada aliyowasilisha 3. Eng. Samwel Hayuma wa TFDA akiwasilisha mojawapo ya mada 4. Meneja Majaribio na Usalama wa Dawa wa TFDA, Bi Kissa Mwamwitwa aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA akitoa hotuba ya ufunguzi.
Msajili wa Dawa Mkuu wa TFDA, Bi. Rose Aaron akisisitiza jambo katika mada aliyowasilisha.
Eng. Samwel Hayuma wa TFDA akiwasilisha mojawapo ya mada
Meneja Majaribio na Usalama wa Dawa wa TFDA, Bi Kissa Mwamwitwa aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA akitoa hotuba ya ufunguzi
Na: James Ndege – Dar es Salaam
Mamlaka ya Chakula na Dawa imekutana na wadau wapatao 50 kujadili udhibiti wa gesi tiba (medical gases) katika ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya TFDA tarehe 16 Agosti, 2018 kwa lengo la
kulinda afya ya jamii.
Mkutano huo umehusisha wadau bidhaa hiyo wakiwemo wazalishaji, waingizaji, wasambazaji, hospitali,
Wizara na taasisi za udhibiti za Serikali kutoka mikoa mbalimbali nchini. Katika mkutano huo, wadau
walijadili na kuelezwa matakwa ya kisheria ya udhibiti wa bidhaa hiyo nyeti kwa afya ya binadamu.
Mamlaka imeanza udhibiti wa bidhaa hiyo ambayo ipo katika kundi la bidhaa za Vifaa Tiba kuanzia
mwezi Aprili 2018 ambapo katika kipindi cha mpito cha mwaka mmoja, wadau wametakiwa kuwasilisha
TFDA orodha na taarifa ya bidhaa walizo nazo kwa utambuzi (notification) na kwamba waanze utaratibu
wa usajili kwa kuwa kipindi cha utambuzi kitamalizika mwezi Aprili 2019 na baada ya hapo bidhaa
ambazo hazijasajiliwa na TFDA hazitaruhusiwa kuingi katika soko.
“TFDA inatarajia wadau wote kukidhi kwa hiyari matakwa ya kisheria ya udhibiti wa gesi tiba kwa muda
uliopangwa ili kuepusha usumbufu usiokuwa wa lazima kwa wale wataokiuka maalekezo haya”, alisema
Meneja wa Majaribio na Usalama wa Dawa, Bi. Kissa Mwamwitwa, aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa TFDA katika hotuba yake ya ufunguzi.
Wadau hao pamoja na TFDA walikubaliana na kuweka maazimio kadhaa kwa lengo la kuwezesha zoezi
husika kufanyika kwa ufanisi, miongoni mwa maazimio hayo ni kuanzisha chama cha wadau wa gesi
tiba, kuboresha Mwongozo uliopo wa udhibiti wa gesi husika na watengenezaji wa bidhaa hiyo kuzalisha
kwa kuzingatia viwango vinavyokubalika ikiwa ni pamoja na kuweka maelezo ya kiusalama katika
bidhaa zao kwa nia ya kulinda afya ya jamii.
Hivyo makala MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA) YAKUTANA NA WADAU KUJADILI UDHIBITI WA GESI TIBA NCHINI
yaani makala yote MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA) YAKUTANA NA WADAU KUJADILI UDHIBITI WA GESI TIBA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA) YAKUTANA NA WADAU KUJADILI UDHIBITI WA GESI TIBA NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/mamlaka-ya-chakula-na-dawa-tfda_16.html
0 Response to "MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA) YAKUTANA NA WADAU KUJADILI UDHIBITI WA GESI TIBA NCHINI"
Post a Comment