Loading...
title : MANYAMA:SERIKALI YA AWAMU YA TANO ITAVUSHA WATANZANIA KWENDA KATIKA UCHUMI WA KATI
link : MANYAMA:SERIKALI YA AWAMU YA TANO ITAVUSHA WATANZANIA KWENDA KATIKA UCHUMI WA KATI
MANYAMA:SERIKALI YA AWAMU YA TANO ITAVUSHA WATANZANIA KWENDA KATIKA UCHUMI WA KATI
Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
WAKILI wa Kujitegemea Leonard Manyama amesema kuwa serikali ya awamu ya Tano chini ya Dk.John Pombe Magufuli itawavusha watanzania kwenda katika uchumi wa maendeleo wa kufanya kazi pamoja na ulipaji wa kodi.
Manyama aliyasema hayo wakati aliposhuka katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akitokea nchini Marekani amesema amejifunza vitu vingi nchini Marekani ambavyo ndivyo Rais Dk.John Pombe Magufuli anapigania katika watu kufanya kazi pamoja na ulipaji wa kodi.
Amesema kuwa ulipaji wa kodi nchini Marekani ni sheria na hakuna majadiliano juu ya ulipaji wa kodi ambapo ndicho kinachofanyika sasa.
Manyama amesema maendeleo yatapatikana tu ikiwa kila mtu atafanya kazi pamoja na kulipa kodi ambayo ndio itafanya maendeleo ya kufikia uchumi wa kati.
Aidha amesema kuwa nchi hii imejaliwa rasimali za kutosha ambazo Rais anazipigania hivyo kila mtu kumuunga mkono kwa vitendo katika kufanya kazi na kusimamia rasilimali zilizopo.
“Nina imani ya Rais kuwa nilichoona nchini Marekani ndicho kinafanyika kwetu katika kuhakikisha kila mtu analipa kodi ambayo sasa indio itafanya mapinduzi katika uchumi wa kati katika uboreshaji wa miundombinu ya barabara , Afya na Mambo mengine mbalimbali”amesema Manyama.
Hivyo makala MANYAMA:SERIKALI YA AWAMU YA TANO ITAVUSHA WATANZANIA KWENDA KATIKA UCHUMI WA KATI
yaani makala yote MANYAMA:SERIKALI YA AWAMU YA TANO ITAVUSHA WATANZANIA KWENDA KATIKA UCHUMI WA KATI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MANYAMA:SERIKALI YA AWAMU YA TANO ITAVUSHA WATANZANIA KWENDA KATIKA UCHUMI WA KATI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/manyamaserikali-ya-awamu-ya-tano.html
0 Response to "MANYAMA:SERIKALI YA AWAMU YA TANO ITAVUSHA WATANZANIA KWENDA KATIKA UCHUMI WA KATI"
Post a Comment