Loading...
title : MARAFIKI WA NMF WAIPA SURA MPYA WODI YA WATOTO YA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA NANYUMBU, MTWARA
link : MARAFIKI WA NMF WAIPA SURA MPYA WODI YA WATOTO YA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA NANYUMBU, MTWARA
MARAFIKI WA NMF WAIPA SURA MPYA WODI YA WATOTO YA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA NANYUMBU, MTWARA
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Nathan Mpangala Foundation (NMF), kupitia programu yake ya Wafanye Watabasamu, hivi karibuni ilishirikisha marafiki wa programu hiyo kubadilisha mwonekano wa wodi ya watoto na chumba cha daktari wa watoto katika Hospitali ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara toka kuta nyeupe na kuwa zenye michoro mbalimbali.
Mwenyekitio wa taasisi hiyo, Nathan Mpangala alisema lengo la kazi hiyo ya siku tano mbali na kuichukulia kama ibada pia ililenga kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuipa wodi ya watoto ya hospitali hiyo mazingira rafiki kupitia sanaa ya uchoraji, kurudisha kidogo walichonacho kwa jamii na kuhamasisha umuhimu wa matumizi ya sanaa ya uchoraji kwenye maeneo yanayotoa huduma ya afya.
“Zahanati, vituo vha afya na mahospitali uhudumia wagonjwa. Mara nyingi huwa na maumivu, uchovu, upweke na msongo wa mawazo. Sehemu hizo zinapokosa michoro ukutani ambayo ingeweza kuwasahaulisha maumivu, hali huwa ngumu zaidi kwao. Sanaa si kwa ajili ya wagojwa tu, ni muhimu pia madaktari, wauguzi na wote wanaohusika na huduma ya afya. Kama maofisini, kumbini, sebuleni, hotelini tunaning’iniza sanaa iweje zinakosekana sehemu nyeti kama mahospitalini?” alihoji Mpangala.
Mpangala anaishukuru Toyota Tz, Shule ya Msingi ya Catton Grove ya Uingereza na marafiki mbalimbali wa NMF kwa kuwezesha tukio hilo na kwamba ametoa wito kwa wadau na wananchi kujitokeza kushirikiana na taasisi yake. “NMF ina mtandao mkubwa wa wachora nchini na wako tayari kujitolea kwa kushirikiana na wananchi au vikundi vilivyo tayari kujitolea.

Marafiki wa Wafanye Watabasamu, kutoka kushoto, Karim Mchaka, Athuman Said, Nathan Mpangala na Ndalo Kalua wakijadiliana jambo wakati wa zoezi la usafi wa jumla katika wodi ya watoto ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara hivi karibuni.
Wanawafanye Watabasamu, kutoka kushoto, Athuman Said, ndilo Kalua na Winny Majuva wakihamisha vitanda kutoka katoka wodi ya watoto ili kupisha uchoraji hivi karibuni.
Kutoka kushoto, George Nyandiche, Neema Loth, Asteria Malinzi na Masoud Kibwana wakiendelea na uchoraji katika wodi ya watoto ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara hivi karibuni.
Wazazi pamoja na watoto wao wakifurahia muonekano mpya wa wodi ya watoto ya Hospitali ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Hamis Dambaya (mwenye shati mikono mirefu) akiwa katika picha ya pamoja na Wanawafanye Watabasamu na baadhi ya viongozi mara baada ya kukamilika kwa uchoraji katika wodi ya watoto Hospitali ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara. (Picha zote na NMF)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MARAFIKI WA NMF WAIPA SURA MPYA WODI YA WATOTO YA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA NANYUMBU, MTWARA
yaani makala yote MARAFIKI WA NMF WAIPA SURA MPYA WODI YA WATOTO YA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA NANYUMBU, MTWARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MARAFIKI WA NMF WAIPA SURA MPYA WODI YA WATOTO YA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA NANYUMBU, MTWARA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/marafiki-wa-nmf-waipa-sura-mpya-wodi-ya.html
0 Response to "MARAFIKI WA NMF WAIPA SURA MPYA WODI YA WATOTO YA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA NANYUMBU, MTWARA"
Post a Comment