Loading...

Mbowe Na Vigogo Wengine CHADEMA Waiomba Mahakama ya Kisutu Isitishe Kusikila Kesi Yao

Loading...
Mbowe Na Vigogo Wengine CHADEMA Waiomba Mahakama ya Kisutu Isitishe Kusikila Kesi Yao - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mbowe Na Vigogo Wengine CHADEMA Waiomba Mahakama ya Kisutu Isitishe Kusikila Kesi Yao, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mbowe Na Vigogo Wengine CHADEMA Waiomba Mahakama ya Kisutu Isitishe Kusikila Kesi Yao
link : Mbowe Na Vigogo Wengine CHADEMA Waiomba Mahakama ya Kisutu Isitishe Kusikila Kesi Yao

soma pia


Mbowe Na Vigogo Wengine CHADEMA Waiomba Mahakama ya Kisutu Isitishe Kusikila Kesi Yao

Na Karama Kenyunko Blogu ya jamii
Viongozi tisa wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi, wamewasilisha maombi  ya kutaka kesi hiyo iharishwe mpaka rufaa yao itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi
Maombi hayo yamewasilishwa leo Agosti 13, 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na wakili wa utetezi Jeremiah Mtobesya mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

Katika maombi yao, upande wa utetezi unaomba mahakama ya Kisutu kuahirisha kesi hiyo mpaka hapo rufaa yao waliyofungua mahakama ya Rufaa itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi

Mapema washtakiwa walikata rufaa kupiga maamuzi ya mahakama Kuu yaliyotolewa mwezi uliopita ambayo yalitupilia mbali maombi yao ya kutaka kesi hiyo ifanyiwe marejeo juu ya uamuzi mdogo uliotolewa na mahakama ya Kisutu

Katika maombi yaliyowasilishwa na wakili wa utetezi Jeremiah Ntobesya na Peter Kibatala wanaiomba Mahakama ya Kisutu iahirishe kesi hiyo hadi Mahakama ya Rufaa itakaposikiliza rufaa yao.

Pia wamewasilisha rufaa ya kutaka kusitisha usikilizwaji wa kesi yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali Mkuu, Mango amesema wamepokea hati ya maombi hayo namba 10.2018 na kwamba wapo tayari kuwasilisha majibu kinzani kesho.

Wakili wa utetezi, Mtobesya naomba wapewe muda wa siku mbili hadi Agosti ilii waweze kufaili majibu ya nyongeza kama watakuwa nayo.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Hakimu Mashauri ameamuru upande wa mashtaka kuwasilisha majibu kinzani Agosti 14.2018 na kama upande wa utetezi watakuwa na majibu ya nyongeza wayawasilishe Agosti 21, mwaka huu.

Maombi hayo sasa yatasikilizwa Agosti 21,2018 na kesi ya msingi nayo pia itatajwa Agosti 21 mwaka huu.

Mbali na Mbowe, washitakiwa  wengine kwenye kesi hiyo ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika.

Washitakiwa wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee,   Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya na Mbunge wa Tarime mjini, Matiko.


Hivyo makala Mbowe Na Vigogo Wengine CHADEMA Waiomba Mahakama ya Kisutu Isitishe Kusikila Kesi Yao

yaani makala yote Mbowe Na Vigogo Wengine CHADEMA Waiomba Mahakama ya Kisutu Isitishe Kusikila Kesi Yao Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mbowe Na Vigogo Wengine CHADEMA Waiomba Mahakama ya Kisutu Isitishe Kusikila Kesi Yao mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/mbowe-na-vigogo-wengine-chadema-waiomba.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mbowe Na Vigogo Wengine CHADEMA Waiomba Mahakama ya Kisutu Isitishe Kusikila Kesi Yao"

Post a Comment

Loading...