Loading...

MKUU WA WILAYA YA CHEMBA ATATUA MGOGORO MATUMIZI YA ARDHI

Loading...
MKUU WA WILAYA YA CHEMBA ATATUA MGOGORO MATUMIZI YA ARDHI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MKUU WA WILAYA YA CHEMBA ATATUA MGOGORO MATUMIZI YA ARDHI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MKUU WA WILAYA YA CHEMBA ATATUA MGOGORO MATUMIZI YA ARDHI
link : MKUU WA WILAYA YA CHEMBA ATATUA MGOGORO MATUMIZI YA ARDHI

soma pia


MKUU WA WILAYA YA CHEMBA ATATUA MGOGORO MATUMIZI YA ARDHI

 Na Shani Amanzi,Chemba.
 
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Saimon Odunga amewataka Wananchi wa Kwamtoro waache tabia ya kuchukua maeneo kiholela badala yake wafate kanuni na taratibu za kuwa na ardhi kwani Serikali inapoteza muda mwingi na pesa katika kuwataftia wananchi maeneo mengine na kuwalipa fidia.

Mhe.Saimon Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa anafanya Mkutano wa Adhara ndani ya siku moja akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chemba,Wataalam wa Halmashauri ya Chemba pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Kwamtoro kwa ajili ya kutatua mgogoro wa ardhi , tarehe 20/8/2018.

Mhe.Saimon Odunga amesema “Wananchi wamekuwa na tabia ya kuvamia maeneo na hata wakipewa maeneo mengine wanatabia ya kuyauza kitendo ambacho siyo kizuru na kusababisha serikali kupoteza muda kuendelea kufatilia nini kifanyike na wengine wanajua kabisa maeneo wanayoyachukua au kukaa ni ya matumizi ya umma kama shuleni,sokoni pamoja na stand ya mabusi”

Aidha amewataka wakazi wa Kwamtoro waliojenga nje ya utaratibu maeneo ya soko,standi na shule watoke haraka sana ndani ya siku 90 na Viongozi wa siasa pamoja na wa Serikali wasipende kutoka nje ya taratibu na kusababisha uchochezi bali fateni taratibu za ardhi kwani Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli inafata kanuni,taratibu na sharia za nchi hasa kwenye ardhi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba amesema Serikali haiwezi kuwaonea wananchi wake ni sawasawa na baba kumuonea mwanae ,badala yake wananchi wanatakiwa kuwa makini na watu wanaowauzia maeneo sa nyingine kwani huwa wanawapotosha kwa kuwauzia maeneo ya umma kitendo ambacho kipo kinyume na taratibu .

Mashimba aliongeza kwa kusema “kwa wale wenye tabia ya kujiegesha maeneo ambayo siyo na kutegemea fidia tabia hiyo waiache mara moja kwani mambo ya kupeleka kesi mahakamani wakati wanajua wapo kinyume na taratibu wanasababisha Serikali kutumia gharama kubwa kuendesha kesi mahakamani na kupoteza muda” .

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba


Hivyo makala MKUU WA WILAYA YA CHEMBA ATATUA MGOGORO MATUMIZI YA ARDHI

yaani makala yote MKUU WA WILAYA YA CHEMBA ATATUA MGOGORO MATUMIZI YA ARDHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MKUU WA WILAYA YA CHEMBA ATATUA MGOGORO MATUMIZI YA ARDHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/mkuu-wa-wilaya-ya-chemba-atatua-mgogoro.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MKUU WA WILAYA YA CHEMBA ATATUA MGOGORO MATUMIZI YA ARDHI"

Post a Comment

Loading...