Loading...
title : MSHINDI MASHINDANO YA MISS TANZANIA 2018 KUJULIKANA SEPTEMBA 8 JIJINI DAR
link : MSHINDI MASHINDANO YA MISS TANZANIA 2018 KUJULIKANA SEPTEMBA 8 JIJINI DAR
MSHINDI MASHINDANO YA MISS TANZANIA 2018 KUJULIKANA SEPTEMBA 8 JIJINI DAR
Na.khadija Seif,Globu ya jamii
Muandaaji wa kinyang'anyiro cha Wanamitindo nchini ambae pia alishawahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1998, Basilla mwanukuzi amezungumza jijini Dar es salaam na wanahabari kuhusu hafla ya mashindano hayo yanayotarajiwa kufikia kilele septemba 8 mwaka huu katika ukumbi wa Julius Nyerere international convention Centre (JNICC).
Aidha Mwanukuzi ametoa shukrani kwa Waziri wa Sanaa,utamaduni na michezo Mh.Harrison Mwakyembe kwa kushirikiana na mashindano hayo tangu yalipoanza mchakato wake April mwaka huu, na kufungua rasmi kwani kulikuepo na changamoto mbalimbali hapo awali likiwemo suala la kufungia mashindano hayo kutokana na sababu mbalimbali, ambapo kimsingi ziliwanyima warembo wengi fursa ya kushiriki.
"Hivyo basi kwa sasa wamepatiwa fursa hiyo na tunategemea tutapata mshindi ambae ataipeperusha bendera yetu Kwenye mashindano ya miss World ambayo yatafanyika nchini China ",alieleza Basilla.Pia ametolea ufafanuzi kuhusu vigezo ambavo vimewekwa bayana kwa mrembo atakaeshinda taji hilo, ikiwemo umri pamoja na uraia wa Tanzania sambamba ukiwekwa mbele zaidi .
Mshindi wa miss Tanzania atapatiwa taji lenye thamani ya shilingi za kitanzania millioni 6 pamoja na gari lenye hadhi nzuri na viwango pamoja na kupata fursa ya kusaidia jamii yake.
Muandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania Basilla Mwanukuzi akizungumzaa na wanahabari jijini Dar es salaam kuhusu mashindano ya warembo hao yanayotarijiwa kufikia kilele chake mwanzoni mwa septemba mwaka huu
Hivyo makala MSHINDI MASHINDANO YA MISS TANZANIA 2018 KUJULIKANA SEPTEMBA 8 JIJINI DAR
yaani makala yote MSHINDI MASHINDANO YA MISS TANZANIA 2018 KUJULIKANA SEPTEMBA 8 JIJINI DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MSHINDI MASHINDANO YA MISS TANZANIA 2018 KUJULIKANA SEPTEMBA 8 JIJINI DAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/mshindi-mashindano-ya-miss-tanzania.html
0 Response to "MSHINDI MASHINDANO YA MISS TANZANIA 2018 KUJULIKANA SEPTEMBA 8 JIJINI DAR"
Post a Comment