Loading...
title : JAMHURI KUWASILISHA MASHAHIDI 34 NA VIELELEZO 15 LIKIWEMO PANGA LINALOTAJWA KUTUMIKA MAUAJI YA MWANAFUNZI SHULE YA SCOLASTICA.
link : JAMHURI KUWASILISHA MASHAHIDI 34 NA VIELELEZO 15 LIKIWEMO PANGA LINALOTAJWA KUTUMIKA MAUAJI YA MWANAFUNZI SHULE YA SCOLASTICA.
JAMHURI KUWASILISHA MASHAHIDI 34 NA VIELELEZO 15 LIKIWEMO PANGA LINALOTAJWA KUTUMIKA MAUAJI YA MWANAFUNZI SHULE YA SCOLASTICA.
Na Dixon Busagaga,MOSHI
JUMLA ya Mashahidi 34 wanatarajia kutoa ushahidi katika shauri la mauaji ya kukusudia ya mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Scholastica iliyopo Himo,Humphrey Makundi.
JUMLA ya Mashahidi 34 wanatarajia kutoa ushahidi katika shauri la mauaji ya kukusudia ya mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Scholastica iliyopo Himo,Humphrey Makundi.
Mbali na Mashahidi hao pia upande wa Jamhuri umepanga kuwasilisha vielelezo 15 vikiwa katika mfumo wa nyaraka pamoja na Panga linaloaminika kutumiwa na mshtakiwa wa kwanza katika shauri hilo.
Hayo yamo katika maelezo ya awali yaliyosomwa jana Mahakama Kuu ,Kanda ya Moshi na Wakili Mkuu wa Serikali,Joseph Pande mbele ya jaji wa mahakama kuu ,kanda ya Moshi,Haruna Songoro.Miongoni mwa mashahidi hao ni baba mzazi wa marehemu,Humphrey,Bw Jackson Makundi,madaktari kutoka hosptali za rufaa za KCMC na Mawenzi,maofisa wa jeshi la Polisi kutoka ofisi ya mkuu wa upelelezi wa mkoa (RCO) na kituo cha Polisi Himo.
Mashahidi wengine ni wahudumu chumba cha kuhifadhia maiti ,hosptali ya rufaa ya mkoa ,Mawenzi na mfanyakazi wa kampuni ya mawasiliani ya simu za mkononi ya Vodacom kutoka Dar es Salaam.Upande wa vielelezo vilivyopangwa kuwasilishwa ni pamoja na simu saba za mkononi zikiwemo za washtakiwa ,ripoti ya uchunguzi wa mawasiliano ya simu pamoja na ripoti ya uchunguzi wa mwili wa marehemu na taarifa ya vina saba (DNA).
Kwa upande wa utetezi unatetewa na wakili Elikunda Kipoko akisaidizana na Wakili Gwakisa Sambo ulieleza mahakama kuwa ushahidi wao utawasilishwa kabla kesi haijaanza.Shauri hilo lilikuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa kosa lao pamoja na maelezo ya mashahidi ambapo washtakiwa wote watatu walikana shtaka lao.
Washtakiwa katika shauri hilo ni pamoja na mlinzi wa shule hiyo Hamisi Chacha ambaye anatajwa kama nshtaliwa wa kwanza,Mkurugenzi wa Shule za Scholastica, Edward Shayo ambaye anatajwa kama mshitakiwa wa pili na Mwalimu wa nidhamu, Laban Nabiswa anayetajwa kama mshitakiwa wa tatu.
Watuhumiwa wa Mauaji ya Mwanafunzi shule ya SCOLASTICA,Himo mkoani Kilimanjaro.
Hivyo makala JAMHURI KUWASILISHA MASHAHIDI 34 NA VIELELEZO 15 LIKIWEMO PANGA LINALOTAJWA KUTUMIKA MAUAJI YA MWANAFUNZI SHULE YA SCOLASTICA.
yaani makala yote JAMHURI KUWASILISHA MASHAHIDI 34 NA VIELELEZO 15 LIKIWEMO PANGA LINALOTAJWA KUTUMIKA MAUAJI YA MWANAFUNZI SHULE YA SCOLASTICA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JAMHURI KUWASILISHA MASHAHIDI 34 NA VIELELEZO 15 LIKIWEMO PANGA LINALOTAJWA KUTUMIKA MAUAJI YA MWANAFUNZI SHULE YA SCOLASTICA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/jamhuri-kuwasilisha-mashahidi-34-na.html
0 Response to "JAMHURI KUWASILISHA MASHAHIDI 34 NA VIELELEZO 15 LIKIWEMO PANGA LINALOTAJWA KUTUMIKA MAUAJI YA MWANAFUNZI SHULE YA SCOLASTICA."
Post a Comment