Loading...
title : Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji Aendelea na Ziara Yake Kutembelea Miradi Mbalimbali. Aagiza Uchunguzi Ufanyika Mradi wa Ujenzi wa Vyumba Vya Madarasa Shule ya Msingi Kigoma.
link : Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji Aendelea na Ziara Yake Kutembelea Miradi Mbalimbali. Aagiza Uchunguzi Ufanyika Mradi wa Ujenzi wa Vyumba Vya Madarasa Shule ya Msingi Kigoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji Aendelea na Ziara Yake Kutembelea Miradi Mbalimbali. Aagiza Uchunguzi Ufanyika Mradi wa Ujenzi wa Vyumba Vya Madarasa Shule ya Msingi Kigoma.
Na.Benny Mwaipaja, WFM, Kigoma
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji,
ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kigoma
kufanya uchunguzi na kuchukua hatua baada ya kubaini
harufu ya ufisadi katika ujenzi wa vyumba vya madarasa 9 ya
shule ya msingi Kigoma yanayojengwa kwa ufadhili wa
Serikali ya Japan kwa gharama ya shilingi milioni 200.
Dkt. Kijaji ametoa maelekezo hayo baada ya Kaimu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Dkt. John Tlatlaa,
kueleza kwamba mradi huo unahusisha ujenzi wa vyumba 10
vya madarasa na vyoo vyenye matundu 12, wakati mkataba
ulioingiwa kati ya Manispaa na Mkandarasi inayoonesha
kwamba yatajengwa madarasa tisa na vyoo vyenye matundu
12.
Baada ya mjadala kati yake na Kaimu Mkurugenzi huyo wa
Manispaa ya Kigoma, akamwelekeza Kaimu Mkuu wa Wilaya
hiyo Bi. Mwanamvua Mlindoko kuchukua hatua za
kiuchunguzi.
"Mradi unaojulikana Mhe. Mkuu wa Wilaya ni wa madarasa
tisa, mkandarasi akija kudai nyongeza ya malipo kwa darasa
moja lililoongezeka atakuwa na haki!, ninachokichukua
mimi ni taarifa hii inayoeleza kujengwa kwa madarasa tisa,
hilo moja ni la kwake Mkurugenzi kichwani" alisisitiza Dkt.
Kijaji
Aidha, Dkt. Kijaji alibainisha kutoridhika kwake na gharama
za ujenzi wa darasa moja kwa shilingi 17m na kwamba kiasi
cha shilingi milioni 200 kilichotolewa na Japan kutekeleza
mradi huo kingeweza kujenga madarasa hata 20.
Awali, akitoa maelezo yake kuhusu ujenzi wa mradi huo
unaojengwa na Kampuni ya Juve Construction and
General Trading ya Mjini Kigoma, Dkt. John Tlatlaa,
alisema kuwa mfadhili, Serikali ya Japan ilitoa masharti ya
majengo hayo kujengwa na mkandarasi badala ya kutumia
nguvukazi-force account.
"Baada ya Japan kutuma fedha hizo na kuingia kwenye
akaunti ya Manispaa tulimwita mkandarasi na kumweleza
kuwa kutokana na wingi wa fedha hizo, atalazimika kuongeza
darasa moja zaidi" alijitetea Kaimu Mkurgenzi huyo.
Maelezo hayo pamoja na ya nyongezwa kwamba majengo
mapya yatawekewa nguzo ndio maana gharama zake ziko
juu, hayakumridhisha Dkt. Kijaji na kuamuru uchuguzi wa
kina ufanyike.
Hivyo makala Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji Aendelea na Ziara Yake Kutembelea Miradi Mbalimbali. Aagiza Uchunguzi Ufanyika Mradi wa Ujenzi wa Vyumba Vya Madarasa Shule ya Msingi Kigoma.
yaani makala yote Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji Aendelea na Ziara Yake Kutembelea Miradi Mbalimbali. Aagiza Uchunguzi Ufanyika Mradi wa Ujenzi wa Vyumba Vya Madarasa Shule ya Msingi Kigoma. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji Aendelea na Ziara Yake Kutembelea Miradi Mbalimbali. Aagiza Uchunguzi Ufanyika Mradi wa Ujenzi wa Vyumba Vya Madarasa Shule ya Msingi Kigoma. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/naibu-waziri-wa-fedha-na-mipango-dkt.html
0 Response to "Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji Aendelea na Ziara Yake Kutembelea Miradi Mbalimbali. Aagiza Uchunguzi Ufanyika Mradi wa Ujenzi wa Vyumba Vya Madarasa Shule ya Msingi Kigoma."
Post a Comment